Header Ads Widget

HUVIKA WATAKIWA KUTUNZA HAZINA AMBAZO MUNGU AMEWEKA NDANI YAO.


Matukio Daima App, Dar es Salaam.

Tumeshuhudia wiki ya Vijana ikiitimishwa, jumapili ya tarehe 20, katika Kanisa KLPT- Kigamboni, huku ikiwa na ujumbe wa Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.


Katika maadhimisho hayo Vijana wametakiwa kutembea kifua mbele na kutoudharau ujana wao bali wawe kielelezo na kuacha kutenda mambo yasiyofaa mbele za Mungu lakini kikubwa kutokuishi katika hofu, ili kujenga imani yao na kutomruhusu Shetani atawale Maisha yao.



Wiki ya Vijana ni wiki ya Utumishi wa Vijana Kanisani ambayo vijana uhusika na mambo yote ya Kanisa ndani ya wiki yao yote, hii haina maana kwamba Vijana hawajishugulishi katika mambo mbalimbali ndani ya Kanisa.


Kanisa la KLPT- Kigamboni ni miongoni mwa Kanisa linatambua umuhimu wa vijana Kanisani na kuamini kuwa kuna hazina iliyowekwa ndani yao, na limekuwa likiitunza hiyo hazina na kuitumia katika kuujenga ufalme wa Mungu ndani na nje ya Kanisa.


Mmoja wa waumini wa Kanisa hilo Mr. Hosea amesema wiki ya Vijana kwa msimu huu imeleta uamsho kwa vijana katika kutumia zile hazina ambazo Mungu ameweka ndani yao, huu ufanyike kuwa mfano kwa Makanisa mengine,  kuwakumbusha vijana Makanisani kuwa wao hawapo kwa jili ya kuimba sifa tu bali kila jambo linalofanyika ndani ya kanisa vijana ndio wenye wajibu wa kushughulika kwa sehemu kubwa kuliko makundi mengine ndani ya kanisa.


 "Kijana asiyehusika katika kanisa kwa jambo lolote huyo hafai kuwepo ndani ya kanisa kwakuwa anakalia kiti cha kanisa na cha Mungu bure na ilehali Mungu alimuokoa kila mmoja ili nae afanye kazi ya BWANA na sio kusinzia ndani ya kanisa. Kumbuka nguvu ya vijana ni siraha ya Mungu kumshinda sshetani"Alisema Hosea 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa HUVIKA, Andrew amewashukuru vijana wa KLPT- Kigamboni kwa kujitoa kwa hali na mali zao, nguvu na kwa muda wao, na amewataka vijana kuongeza juhudi katika kumtumikia Mungu, kwani kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa.



"Mungu awabariki sana wito wangu ni kwamba vijana wengi zaidi wajitokeze kwenye matukio tunayoyapanga, zikiwemo semina na matamasha mbalimbali ili kujijenga kiroho na kimwili pia" alisema  Andrew.


Umoja wa Vijana Kanisa la KLPT- Kigamboni (HUVIKA) wamefanya mambo mbalimbali kama vile kufanya shughuli ndani ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na kurekebisha muonekano wa mbele wa Madhabahu na kutoa shukrani kwa wazee na wachungaji.


Kufanikiwa kwa wiki ya Vijana kunatokana  na tabia ya vijana kuwa na tabia ya kujihusisha katika jambo ambalo kila mmoja binafsi anaona anaweza kulifanya na hivyo kuwa ni sehemu yake ya kumtumikia Mungu ndani ya kanisa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI