Header Ads Widget

HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA YAPATA SULUHU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


HOSPTALI ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa (BMH) imeanza matibabu ya kutibu wanaume wenye changamoto za nguvu za kiume kwa kutumia njia ya vipandikizi vya Uume.


Mkurungezi Mtendaji wa Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa Dkt Alphonce Chandika ameyasema hayo leo Jijini hapa wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu vipaumbele vya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023-2024


Aidha Dkt Chandika Amesema ,huduma hiyo ya upandikizi ilianza mwezi Juni, 2022 ambapo mpaka sasa tayari wameshafanya upandikizi kwa wagonjwa wawili.


"Kwakweli matokeo ni mazuri kwani wagonjwa waliofanyiwa upandikizi wameleta ushuhuda na kubainisha kwamba wanaendelea vizuri na zoezi zima la uzalishaji rasilimali watu, "Amesema Dkt Chandika.


Hata vivyo amesema Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa ipo kwenye harakati ya kuhakikisha huduma hiyo ya upandikizi (Uume) inapatikana muda wote na kushauri Hospitali zingine ziwe na huduma kama hiyo kwani tatizo ni kubwa.


Akieleza vipaumbele vichache Kati ya vingi vilivyopo katija bajeti ya Mwaka huu ni Kuifanya BMH kuwa Hospitali ya pili Taifa kwani Hospitali hiyo inahudumia wananchi zaidi ya milioni 10 wa Mikoa ya Dodoma, Iringa, Singida, Manyara, na baadhi ya Maeneo ya Mikoa ya Morogoro na Tabora.


Amesema pia wanapokea wananchi kutoka karibu kila kona ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania wanaokuja kufuata huduma za matibabu ya kibingwa na ubobezi .


Pia ameeleza kwa Mwaka huu wa Fedha wametengewa Shilingi Bilioni 64.52 ambapo Shilingi Bilioni 18.62 zinakwenda kwenye miradi ya Maendeleo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri Mbali kupata matibabu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI