NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANANCHI wa kata za Mwika kusini na Mwika kaskazini katika Jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wanaenda kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji safi ambapo miradi miwili yenye thamani zaidi ya Bilioni 2.5 inaenda kutekelezwa.
Hatua hii imemuja kutokaba na uchapakazi mkubwa wa Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt . Charles Kimei ndani ya Bunge na ufuatiliaji mahiri wa utatuzi wa kero ya maji kwa wananchi wake.
Ikumbukwe pia Dkt Kimei alimuomba Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aweze kutembelea Jimbo la Vunjo na kujionea changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo alifika na kutembelea vyanzo vya maji vya Mwika Kaskazini ambavyo ni Marua A spring, Marua B spring, Kwasongoro spring, Mseke Spring, Lyanyori A, Lyanyori B na Mtiro Kondiki.
Pamoja na kufanya mkutano wa wananchi katika kata ya Njiapanda ambako aliahidi kuwa mbunge wa pili wa Jimbo la Vunjo kwa kuhakikisha anasaidia utatuzi huo.
Waziri Aweso kama kawaida yake ni mtu muungwana na mkweli aliyedhamiria kwa vitendo kuona malengo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama Ndoo kichwani yanafanikiwa aliahidi kutoa fedha za kumaliza changamoto ya maji Jimbo la Vunjo ikiwa ni utekelezaji wa ibara ya 100 ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Kupitia mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Moshi, MUWSA serikali kupitia wizara ya maji ilitoa bilioni 2.3 kutoa maji Miwaleni kwenda Njiapanda, shilingi milioni 500 mradi wa maji kata tatu za Kilema Kaskazini, Kilema Kati na Kilema Kusini kupitia RUWASA.
Pia ikatoa shilingi bilioni 2.1 mradi mkubwa wa maji kupitia RUWASA vijiji 11 vya kata za Marangu Mashariki na Marangu Magharibi.
Aidha kunatekelezwa mradi wa shilingi milioni 300 kwa ajili ya upanuzi wa huduma kwa wananchi katika kata ya Makuyuni na shilingi milioni 226 katika kata ya Marangu Mashariki vijiji vinavyohudumiwa na MUWSA kama vile Samanga na Rauya.
Sasa imekuwa zamu ya Mwika Kaskazini ambako kutatekelezwa mradi wa maji wa shilingi bilioni 1.7 na Mwika Kusini shilingi milioni 861 katika mwaka huu wa fedha 2023/24.
Tayari shehena ya mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yote hiyo yameshapokelewa na kazi hiyo itaanza wiki ijayo.
"Tunajivunia uwakilishi wa Mbunge wetu Dkt Charles Stephen Kimei na tunaona fahari ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan tunamshukuru na kwa pamoja tutaendelea kuwaamini na kuwaunga mkono ni waumini wa kweli wa siasa za maendeleo".
0 Comments