Header Ads Widget

BODI YA RUWASA TAIFA YAVUTIWA NA MRADI WA MAJI MKUMBWANYI IRINGA

 


Mwenyekiti wa RUWASA Taifa Mhandisi Ruth Koya (Kushoto) akimtwisha Ndoo ya Maji mwanamke mkazi wa Migoli Iringa Leo 

................................................................

Na Matukio Daima APP,Iringa 

MWENYEKITI wa bodi ya Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Taifa Mhandisi Ruth Koya amepongeza jitihada za RUWASA Wilaya ya Iringa vijijini kwa usimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Maji Mkumbwanyi Kijiji cha Makatapola Wilaya ya Iringa.

Mhandisi Koya ametoa pongezi hizo Leo wakati wa ziara ya bodi ya RUWASA kukagua Miradi ya Maji katika Wilaya ya Iringa vijijini  .

Alisema bodi yake imeridhishwa na Ujenzi wa mradi wa Maji wa  Mkumbwanyi Kijiji cha Makatapola Jimbo la Isimani Wilaya ya Iringa vijijini kuwa ni mradi ambao ni Mzuri utakaomaliza kero ya Maji kwa wananchi wanaozunguka mradi huo .

Mhandisi Koya alisema lengo la Serikali ya awamu ya sita inayoonhozwa na Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan ni kumtua mama Ndio kichwani na Ndio maana Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi za kutekeleza Miradi ya Maji ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM .

Hivyo alisema bodi ya RUWASA imeendelea na ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji nchini lengo ni kuthaminisha ubora wa Miradi hiyo na fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maji nchini .


Hata hivyo aliwaomba wananchi kuendeleza kutunza mazingira Ili kuifanya Miradi hiyo kuwa endelevu zaidi .

Mapema msimamizi wa taarifa ya mradi wa Mkumbwanyi Msimamizi wa Maji Kata ya Migoli Lilian Dominick alisema mradi huo utahudumia walengwa 6138 na  utekelezaji wa Ujenzi wa mradi  umefikia asilimia 100 na tayari Mkandarasi wa mradi huo M/S GNMS Contractors co.Ltd ameshalipwa fedha zake kwa asilimia 100 na kuwa gharama ya mradi ni shilingi bilioni 1,787,500,191.

Huku meneja wa RUWASA Wilaya ya Iringa Exaud Humbo alisema kuwa lengo la RUWASA ni kuwafikia wananchi wengi zaidi kupata huduma ya Maji na Sasa wameanza kununua Mita Ili kuzifunga kwa watumiaji kwa lengo la kuthibiti upotevu wa Maji na Jumla ya Mita 3500 zinakusudiwa kufungwa.

Hata hivyo alisema wamefanikiwa kuongeza makusanyo yatokanayo na Maji kwa Vyombo Vya watumiaji Maji ndani ya Wilaya ya Iringa .

Alisema kuwa jumuiya ya watumiaji Maji Kihwele inaongoza kwa ukusanyaji wa mapato ikifuatiwa na jumuiya ya migoli.

Pia alitaja changamoto kuwa ni pamoja na wananchi kuharibu kusudi Mita za Maji Ili kuendelea kupata Bure huduma hiyo kwa madai Maji ni Tunu Toka kwa Mungu hawapaswi kulipia .

Alisema kutokana na changamoto hizo wameendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa Wilaya na chama Tawala .

Akishukuru kwa niaba ya wananchi diwani wa viti maalum tarafa ya Ismani Yusta Kinyaga alimpongeza Mwenyekiti wa bodi ya RUWASA kuhusu ushauri wake wa kutazama gharama za Maji zisizomuumiza wananchi .

Pia alimshukuru Mbunge wa Ismani William Lukuvi kwa kupigania Miradi hiyo ya Maji .

Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Taifa na wajumbe wakikagua mradi wa Maji Mkumbwanyi 






wajumbe wa bodi ya RUWASA Taifa wakiwa katika picha ya pamoja 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI