Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
BODI ya Mkonge Tanzania imesema imeagizwa na Serikali,kuhakikisha kuwa uzalishaji wa Mkonge unaongezeka hadi kufikia Tani 120,000 kwa Mwaka, ifikapo Mwaka 2025/2026.
Hayo yalibainishwa Leo Agosti 16 Jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saddy Kambona wakati akizugumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa odi hiyo a mwelekeo katika mwaka huu wa fedha.
Amefafaua kuwa hatua za serikali kuliingiza zao la mkonge kwenye orodha ya mazao ya kimkakati ilitokana na ukweli kwamba mahitaji na soko la mkonge limezidi kuimarika Duniani.
“Hii ni kutokana kugundulika kwa matumizi mapya ya mkonge na uzalishaji wa bidhaa mpya zitokanazo na mkonge kama vile vifaa vya ujenzi, Matofali,mbao, mabati, vigae), Sukari ya Mkonge, Pombe ya Mkonge, Karatasi maalum, Bio Gas, mbolea, Chakula cha mifugo , urembo, mabodi ya magari,”ameeleza.
Hata hivyo ametaja Wilaya zilizopatiwa mbegu hizo ni Korogwe, Muheza, Tanga, Mkinga, Handeni, Kilindi, Rorya, Bunda, Butiama, bariadi, Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Manyoni, Singida Vijijini na Mkalama
Aidha amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwakutoa fedha kwa ajili ya kununua mitambo mipya ya kuchakata Mkonge na kufufua mitambo ya kuchakata mkonge ya mashamba ya Kibaranga Wilayani Muheza, Tanga na shamba la serikali la TPL lililopo Kata ya Bwawani Wilayani Arumeru, Arusha ambalo linasimamiwa na kuendeshwa na TSB.
“Mitambo hii itasaidia sana kuongeza uzalishaji wa Mkonge na hivyo kuwezesha kufikiwa kwa lengo la uzalishaji lililowekwa na serikali,”amesema.
Na kuongeza "Nimpongeza Rais Dkt, Samia kwa hatua za kimageuzi alizochukua na anazoendelea kuchukua katika kuleta mageuzi ya kweli kwenye zao la mkonge na sekta ya kilimo kwa ujumla," Amesema Kambona






0 Comments