Header Ads Widget

BENKI YA UCB YAPATA FAIDA 100% KWA MWAKA 2022.



Matukio Daima App, Kilimanjaro.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania KKKT  Askofu Dkt Fredrick Shoo  amesema kuwa mwenendo wa Benki ya uchumi UCB inaendelea kuimarika na kukua  kwani imeweza  kuongeza faida na rasilimali za bank kwa asilimia 100 kwa kipindi Cha mwaka 2022. 


Mkuu wa Kanisa Dkt Shoo  ambaye  pia ni mwana hisa katika benki hiyo amebainisha hayo kwenye mkutano mkuu wa 17 wa wanahisa wa Bank ya Uchumi uliofanyika Mkoani Kilimanjaro 


Aidha Dkt. Shoo amewataka wanahisa kuhakikisha wanaendelea kuwekeza Kwenye bank ya Uchumi Ili kukuza mtaji wa bank na kuiwezesha kufikia malengo na kuwa bank ya kibiashara.


"Leo tumekuwa na mkutano wa kupokea Taarifa ya benki yetu na na tumeridhishwa na Taarifa ambayo tumeipewa lakini pamoja na changamoto zilizopo Kuna haja ya kuongeza hisa ili kuendelea kuboresha zaidi "Alisema Doct.Shoo.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wanahisa wa Benki hiyo na wasio wanahisa kuendelea kununua hisa  katika benki hiyo ili kuendelea kikuza benki hiyo.


Kwa upande wake meneja wa Benki hiyo ya Uchumi Samuel wado amesema kuwa Benki hiyo imeendelea kukua na kuongeza faida kwa asilimiamoja kwa mwaka 2022.

Amesesema kuwa mkakati waliojiwekea Cha miaka mitano ni kujikita katika kikuza mtaji wa Benki na kusema kipindi Cha nyuma benki haikuweza kuongeza mtaji kama inavyotakiwa.


"Kwa sasa wanahisa wameendelea kishauri ujenzi wa matawi ya benki katika maeneo mbalimbali ili kiwezesha huduma hiyo katika maeneo mbalimbali kupatika kirahisi"


Amesema kuwa Wanahisa wamependekeza kuweka mipango mkakati wa utoaji wa huduma ili kuendelea kuwafukia wateja na kuboresha huduma za kidigitali ili wateja waweze kufikiwa kwa wingi ma kwa uragisi.

Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo amesema kuwa  pamoja na changamoto za mfumuko wa benki uliotokana na uviko 19 na vita ya Ukrein kwa mwaka 2022 Benki imeendelea kuimarika na kufanya vizuri.


"Benki imeendelea kuboresha huduma na kuongeza maeneo ya kutolea huduma kama kule himo. Malengo ya kimkakati na mtaji wa benki. Mwaka 2022 Katika kutekeleza Mpango mkakati wa 2018/2022 kiwango cha kuongeza mtaji hakikuweza kufikiwa cha bilioni 15"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI