Header Ads Widget

WAZIRI ULEGA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE MKURANGA , ATOA MAAGIZO KWA HALMASHAURI

 



Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ameagiza shule ya msingi mpya ya Maliasili iliyopo katika kijiji cha Kamegele Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Watoto wa darasa la kwanza hadi la tatu waanze kusoma mapema mwaka huu badala ya kusubiri hadi mwakani ilikusaidia wasitembee umbali mrefu kufuata Shule.


Ametoa agizo hilo wakati alipofika katika kijiji cha Kamegele kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule za msingi na Sekondari zilizojengwa baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotoa kibali cha kumega eneo la msitu wa Vikindu ilikujengwa  shule hizo ambapo pia Ulega alikabidhi madawati 100  kwaajili ya maendeleo ya shule hizo.


Ulega alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo kukaa na wataalamu wake wa Halmashauri hiyo kuangalia namna bora ya kuwasaidia watoto wadogo ambao hutembea kutoka kijijini hapo hadi shule za msingi Mwandege na Vikindu umbali wa zaidi ya kilomita kumi kufuata Shule huku shule ambayo wakejengewa na serikali ya awamu ya sita ipo hatua za mwisho kukamilika.


Awali akitoa maelezo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge huyo wa Jimbo la Mkuranga Mkurugenzi huyo alisema shule hiyo itafunguliwa mwakani na ndipo Mheshimiwa Ulega alitoa agizo hilo kwa kusema kusubiri hadi January mwakani ni mbali sana na Watoto wanateseka kwa kwenda umbali mrefu kufuata Shule.


"Wapo watoto wadogo wanaosafiri umbali mrefu sana kufuata Shule Wapo wanaokwenda Shule ya msingi Vikindu, Kisemvule, Mwandege ambako ni mbali sana nami nakubali tunaweza kuifungua shule January mwakani lakini hivi vitoto vidogo ndio viendelee kusubiri hadi mwezi wa Kwanza mwakani? Alihoji Mheshimiwa Ulega


"Nisikilize Mkurugenzi hivi vitoto vidogo dogo vya darasa la kwanza, la pili na la tatu vinavyotembea umbali mrefu kaachini na wataalamu wako njooni muangalie wapo wangapi wanaotoka huku kwenda kule mbali waanze kusoma" 


Ndipo Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga alipokea agizo hilo kwa kuahidi kulifanyia kazi agizo hilo huku Wananchi wakishangilia kwa kupiga makofi na vigelegele.


Mheshimiwa Ulega alisema "Rais Dr Samia Suluhu Hassan Mama yetu kashajenga shule hii hapa fanya linalowezekana Watoto waanze kusoma Mimi ntaongezea madawati mengine mia moja utaanza nayo ili shule ianze" 


Aidha aliwasihi Wananchi wa Kijiji cha Kamegele waendelee kuwa wavumilivu kwa kumpa nafasi Mkurugenzi na wataalamu wake kulifanyia kazi agizo hilo wataleta jibu.


Hatahivyo Waziri huyo na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga alimshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa fedha za ujenzi wa Shule za msingi na Sekondari katika eneo la kijiji hicho kwani wazazi pia wamekuwa wakigharamika kulipa boda boda ya zaidi ya shilingi 6000/- kwa siku ili waende shule au Watoto wao watembee umbali huo wa kilomita kumi kufuata Shule.


"Sisi tuliomba eneo la msitu tujenge shule lakini Mama yetu kwa upendo mkubwa ametupatia fedha za kujenga shule ya Sekondari na ya msingi sio jambo dogo jamani, shule ya Sekondari kidato cha kwanza wameshaanza kusoma na hii msingi sio muda mrefu wataanza kusoma" 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI