NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) kupitia ofisi ya Kanda ya ziwa imewataka watumiaji wa huduma hiyo kuhakikisha wanakata bima zenye viwango na kuachana na tabia ya ukataji wa bima chini ya kiwango.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya ziwa Richard Toyota alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi Kwa waandishi wa habari Kwa kipindi Cha mwaka mmoja kuanzia julai 2022 Hadi juni 2023.
Toyota ameeleza kuwa ununuzi wa bima chini ya kiwango husababishwa madhara mbalimbali ikiwemo kutolipwa fidia Kwa wakati, kulipwa fidia Ndogo tofauti na mteja alivyostahili kulipwa pamoja na kuhusika kudhoofisha juhudi mathubuti za serikali katika kutoa huduma stahiki Kwa wananchi.
Aidha ameeleza kuwa Kwa kipindi Cha septemba 2022 Hadi kufikia Februari 2023 wamefanya ukaguzi wa bima katika vituo vya mafuta 252 Kwa mikoa mitano na kubaini vituo 158 sawa na Asilimia 63 havikuwa na bima ya majanga.
Toyota amefafanua kuwa katika ukaguzi huo Mkoa wa Mwanza unaongoza Kwa kuwa na vituo vya mafuta 61 sawa na Asilimia 39 visivyokuwa na bima ya majanga huku vituo 32 sawa na Asilimia 34 ya vituo vyote, 94 vyenye bima vilikata bima chini ya kiwango ambapo ni kinyume na Tangazo la serikali namba 251 la mwaka 2018.
"Hatua stahiki Kwa watoa huduma zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa Kwa mujibu wa sheria na walaji wa bima yani wamiliki wa vituo" Alisema Toyota.
Amesema kuwa katika kuhakikisha sheria ya bima na sheria ya mafuta zinasimamiwa ipasavyo Ewura inapaswa kuwachukulia hatua wale wote wanaojaribu kukengeuka.
"Na Kwa taarifa tulizonazo tayari Ewura wameanza kuchukua hatua zinazostahili Kwa wale wote walivunja seria" Alisema Toyota.
Ukaguzi huo wa bima kwenye vituo vya mafuta umefanyika katika Mikoa ya Kigoma ( Wilaya ya Kasulu), Shinyanga, Geita na Mara.
0 Comments