Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Tanga.
WATU 11 waliokuwa wameweka kambi maeneo ya Donge Mkoani hapa wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Tanga kwa makosa ya wizi wa njia ya mtandao ya simu.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga(RPC) Hendry Mwaibambe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwa watuhumiwa hao wamekutwa na fedha shilingi za Tanzania,Dola za Marekani na fedha za Congo DRC,simu,line,jiko la kuchomea line za simu baada ya kuzitumia, orodha ya namba walizolikwishatapelia na wanazotarajia kuendesha utapeli huo.
Kamanda Mwaibambe alisema baada ya kuwahoji kwa muda mrefu watuhumiwa hao walikiri njia walizokuwa wanazitumia kutapeli ambapo walikuwa wanawapigia watu au kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa ajili ya kutumiwa pesa au kuomba namba za siri.
Alisema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi katika makazi yao walikutwa na vitu mbalimbali ikiwemo kadi za simu,pikipiki,kadi za benki simu ndogo za tochi 13 za aina mbalimbali,simu 11 kubwa za smartphone
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amewataja waliokamatwa na kuhusishwa na utapeli huo kuwa ni Hadija Nyange (34) mkazi wa Muheza,Zaina Athumani (25) mkazi wa Mwanzange,Innocent Omeme (35) wa Dar es salaam,Abdulaziz Nzori (31) wa Dar es salaam, Said Hassan (24) wa Dar es salaam, Rashid Habibu (23) wa Dar es salaam,Said Juma (30) ,Idd Kaniki (35),David Rupiana wa Dar es salaam (22),Omary Mohamed (27) wa Mkanyageni Tanga na Salum Rajab (24) wa Dar es salaam.
Alisema watuhumiwa hao wanadaiwa kuendesha uhalifu katika mikoa mbalimbali hapa Nchini na kuwaomba wananchi watoe ushirikiano na Jeshi la Polisi ili kuweza kukabiliana na wahalifu hao ili waweze kuchukuliwa sheria kali na tayari Jeshi hilo limekwisha wafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
0 Comments