Header Ads Widget

WATOTO WAWILI WA KIKE WAZALIWA KWA UPASUAJI SIKU YA KWANZA YA KUANZA KITUO CHA AFYA MAKOWO NJOMBE.

Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Mhe.Deo Mwanyika

Diwani wa kata ya Makowo Honolatus Mgaya (Luketulo)



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Hatimaye kituo Cha Afya Makowo kilichopo Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe kilichojengwa kwa miaka mitano kimeanza rasmi kutoa huduma za afya kwa wananchi.


Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kubeja Ganja amesema Hadi sasa Kuna vituo vya afya vinne katika Halmashauri hiyo ambavyo ujenzi wake ulianzishwa na wananchi pamoja na mapato ya ndani na hivyo wananchi wa maeneo mbalimbali wataanza kupata huduma hapo huku Mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dokta Isaya Mwasubila akiwataka wataalamu na wananchi kulinda vifaa tiba vilivyopo.


Diwani wa kata ya Makowo Honolatus Mgaya amesema haikuwa Kazi rahisi kukamilika kwa kituo hicho Cha afya kwani amegombana sana na mganga mkuu Hadi sasa kituo hicho kimeanza kufanya kazi na tayari huduma za upasuaji nazo zimeanza kwa kufanikiwa kuzalisha watoto wawili wa kike ambao mmoja wa kwanza amependekeza aitwe Samia.


Jumla ya watumishi 9 wa afya wamepelekwa katika kituo hicho cha afya ambapo mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika akiwa katika ziara yake ya kikazi amewataka wananchi kuishi nao vizuri ili wawahudumie huku akimshukuru Rais kwa kupeleka fedha,vifaa tiba na wataalamu.


Baadhi ya wananchi wa Makowo akiwemo Yolanda Kipeta Lusius Galus na Genofesa Msemwa wamekiri kurahisishiwa upatikanaji wa huduma za afya kwani wamekuwa wakitembea umbali wa Km 90 mpaka Njombe mjini na kwa gharama kubwa kufuata huduma za afya.


Takribani shilingi milioni 600 zimetumika kujenga kituo cha afya Makowo katika kipindi cha miaka mitano hadi sasa kimeanza rasmi kutoa huduma za afya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI