Header Ads Widget

WAKULIMA NYANDA ZA JUU KUSINI WACHANGAMKIA FURSA YA UUZAJI MAHINDI CPB KWA BEI KUBWA

 

KASI ya  wakulima   wa  mikoa ya  nyanda  za  juu  kusini  kuuza mahindi yao  bodi  ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB)   ni zaidi ya  asilimia 95   kutokana na bei  nzuri  asilimia  ya  ununuzi  wa mahindi katika  bodi  hiyo   iliyoongezwa na  serikali kwa  kutoa  fedha za  kutosha za  kununua mahindi ya  wakulima .



Meneja  wa  CPB  kanda ya  nyanda  za  juu  kusini  Dkt  Jaspa Samweli alimweleza  mwandishi wa matukio Daima Media  leo   kuwa   ongezeko  la  wakulima    wakubwa na  wadogo  kuuza mazao  kwa  sasa  ni  kubwa  zaidi  kwani  imepelekea  zoezi la  ununuzi wa mahindi kuongezwa  kasi  zaidi  ikiwa ni pamoja na kuongeza  vituo  vya  ununuzi wa mahindi hayo katika mikoa ya  Singea   mkoa  wa   Ruvuma ,  Mlowo  na Tunduma  mkoa  wa  Songwe   Songwe  pamoja na Iringa .

Alisema  kuwa  CPB imeanza  kununua  mahindi  mwezi  mmoja  uliopita  kwenye kituo cha Iringa kwa  Julai 24  bei ya mahindi  kwa kilo moja  ni   kiasi cha  shilingi 950 wakati  kituo  cha Songea  kwa  kilo  ni shilingi 850 kwa  kilo kituo cha Mlowo na  Tunduma mkoani  Songwe  kilo  moja  ni shilingi  850  .


 Alisema  kuwa   hadi sasa  zaidi ya  tani za mahindi ya  wakulima 13,500 zimekwisha  nunuliwa  kati ya  tani 80,000 zinazotarajiwa  kununuliwa  kutoka kwa  wakulima  ndani ya  mikoa  ya nyanda za  juu  kusini .

Hata   hivyo  alisema  kutokana na  ongezeko  kubwa la  wakulima  kukimbilia  kuuza mahindi yao  katika    ofisi  za  CPB Iringa   wamelazimika   kuweka  utaratibu  wa  kununua mahindi  hayo  kutoka kwa  wakulima  wa gunia  mpoja   hadi  tani  mbili na  wale  wakulima  wakubwa  wa tani  saba na  kuendelea  ambao  wanafika  kuuza mahindi yao .


Alisema  kwa  wote wanaofika  kuuza mahindi  yao  kuwa  viwango  vya ubora  wa mahindi  yanayotakiwa  kununuliwa  hivyo kabla ya  ununuzi  mahindi yanapimwa maabara  na  yale  yaliyokidhi  viwango  yananunuliwa   kwa  mkulima  kuingiziwa  pesa  yake  katika akaunti ya  benki zoezi  ambalo  linachukua  muda  mfupi  zaidi toka  ununuzi
  hadi  kuingiziwa pesa ni ndani ya  silku tatu  pesa inakuwa tayari kwenye  akaunti ya  mkulima .


Dkt  Samweli  alisema  kuwa  eneo  la  ununuzi wa mazao  linauwezo  wa kupokea magari 50  kwa  wakati mmoja  japo kwa  sasa  magari yanayoingia  kwa  wakati  mmoja ni kati ya 100 na  zaidi  hivyo  wameweka  utataribu  mzuri  wa  kuona  kila mkulima  anauza mahindi yake  CPB kwa wakati  zaidi .

Alisema  wakulima  wanaofika  kuuza mahindi  baada ya  kufika  mahindi  yanachukuliwa  sambo pamoja na namba ya  gari  jina la dereva na  namba yake ya  simu  kisha  dereva  anaruhusiwa  kwenda  kuegesha  gari lake  sehemu  yoyote  ndani ya mji wa  Iringa na  pale  majibu ya  vipimo  vya maabara  yatakapotoka  dereva anapigiwa  simu  ili  kuingiza  gari kwa  ajili ya upakuaji wa mzigo  na  wale  ambao  watakuwa  hawajakidhi  vigezo  kwa mahindi yao  kukosa  ubora  wamekuwa  wakijulishwa  ili  kwenda  kutafuta  soko sehemu  nyingine .

Dkt  Samweli  alisema kuwa  mwitikio  mkubwa  wa  wakulima kufika  kjuuaza mazao yao kwao ni kutokana na  bei  nzuri ya  ununuzi wa mahindi kwa kilo kwani mtaani  wafanyabiashara  wananunua mahindi kwa  kilo  kwa  kiasi cha shilingi 650 kwa  kilo    hivyo  alisema  bado  anatoa  rai kwa  wakulima na wafanyabiashara  kuendelea  kutumia  fursa ya  kuuza mahindi CPB bora   mahindi yawe na  ubora .

Alisema  CPB  ina jumla ya  vipimo 12  vya   kupima  ubora  wa mahindi yanayonunuliwa  ili  kuendena na  soko la mahindi  la  Afrika Mashariki  ili  kuepuka  kulichafua  Taifa  kwa  kupeleka  mahindi  ama  unga  usio na ubora katika  soko la Afrika Mashariki .


"  Uandaaji  wetu  wa mahindi  toka  kwenye  ununuzi hadi  usagaji  ni uandaaji  wenye  viwango  vya  soko la Afrika  mashariki  ambao  unatumiwa na nchi  zote  za Afrika  mashariki  pia  alisema mfano  unga   unaotoka  CPB ni  unga  wenye  virutubisho   vyote na unga  usio na madhara ya Sumu  kuvu "


Alisema  kama  mahindi ama   unga  ama  maharage na  mazao  mengine  yanayotoka   Tanzania  yakipelekwa  nje ya  nchi na  kubainika  kuwa na tatizo  aibu  hiyo  si ya  wakulima  ama CPB pekee yao  bali ni aibu kwa  Taifa  zima  na atakayeangaliwa na Rais  wa nchini ya  Tanzania  Dkt  Samia  Suluhu Hassan  na  sio  mkulima ama CPB   hivyo ni jukumu lao  kuendelea  kulinda  taswira ya  nchi kwa  kuzingatia  ubora  wa mazao yanayonunuliwa na  kuuzwa nje ya  nchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI