Header Ads Widget

"UWEKEZAJI WA BANDARI UPO KWENYE ILANI YA CCM"_ CHONGOLO.




Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Tanga. 


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Daniel Chongolo amesema Rais Dk Samia Suluhu na Serikali yake anatekeleza ilani ya Chama hicho ya mwaka 2020/2025 katika miradi mkakati na swala la uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam sio jambo jipya kama watu wanavyolitafsiri.


Kauli hiyo ameitoa July 19 kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika Wilayani Korogwe Mkoani hapa mkutano uliokuwa na malengo ya kutoa darasa la elimu juu ya mchakato wa swala la uwekezaji wa Bandari baina ya Kampuni ya Dubai Ports World (DP WORLD) na Serikali ya Tanzania.


Chongolo alisema ilani ya chama hicho ya miaka mitano kuanzia 2020 hadi 2025 imeweka wazi miradi mkakati ambayo inapaswa kutekelezwa ikiwa pamoja na Reli, Ndege,maswala ya anga,bahari sambamba na ununuzi wa vyombo vya usafiri na kuimarisha huduma ya bandari ya Dar es salaam kwa ujenzi wa baadhi ya magati.


"Jambo hili linavyojadiliwa ni kama jambo jipya lakini lipo kwenye ilani yetu ya ccm ya 2020/2025 na Rais wetu anateleza tu kama anavyotekeleza miradi mingine ile ya bwana la Mwalimu Nyerere, daraja la busisi,Reli ya Standard gaje n.k"Alisema Chongolo.


Alisema Serikali imekusudia kuimarisha huduma katika Bandari hiyo ambayo itakuwa kichocheo kikubwa cha mapato ya Taifa yatakayoifanya Serikali kutokutegemea fedha za wahisani ambazo zinatolewa kwa masharti magumu.


Aidha alisema wananchi wanapaswa kufahamu kuwa Serikali ipo katika vita kubwa ya kiuchumi kuliko ile ya ukombozi na ni vita ambayo inamalengo ya kutaka  kuzorotesha jitihada zinazofanywa na Serikali ili Nchi isiweze kujitegemea kiuchumi.


Akizungumza katika Mkutano huo Waziri wa uwekezaji Prof Kitila Mkumbo alisema ili Nchi iweze kukua kiuchumi lazima kuwepo na mwekezaji kwa upande wa Serikali au Sekta binafsi na hiyo ndio dhana na faida ya uwekezaji. 


Prof Mkumbo alisema changamoto inayoikabili Bandari ya Dar esa Salaam ni pamoja na uwezo mdogo wa kuhudumia jambo ambalo Serikali inawajibu wa kutenga zaidi ya Tirioni 3 toka vyanzo vya ndani ili kufanyike maboresho jambo ambalo linaweza kuathiri huduma za kijamii.


Alisema ukaribishwaji wa muwekezaji toka Kampuni ya Dubai Ports World (DP WORLD) kutakuwa na faida nyingi mojawapo Serikali haitawajibika kufanya maboresho yoyote ambayo yangeigharimu Nchi na kupelekea kwa baadhi ya huduma muhimu za kijamii kukwama.


"Watu wanazungumza mambo mengi lakini Serikali iko makini sehemu zote nyeti zitaendelea kumilikiwa na Serikali kupitia mamlaka zake hasa swala la umiliki wa bandari na Ulinzi na usalama vyote hivi vitaendelea kusimamiwa na Serikali "Alisema Prof Mkumbo. 


Kwa upande wake Naibu waziri wa Uchumuzi Atupele Mwakibete alisema wapo watu wanao wadanganya wananchi ya kuwa bandari zote zitachukuliwa na Kampuni ya Dubai Ports World jambo ambalo sio la kweli na linatakiwa kupuuzwa.


Alisema uwekezaji unaotakiwa kufanywa baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni hiyo unahusu bandari ya Dar es salaam tu tena kwa baadhi ya maeneo na utekelezaji huo ndio utakao pelekea kujenga ushawishi kwa Nchi za jirani kutumia bandari hiyo ambayo itakuwa na ufanisi mkubwa kiutendaji baada ya uwekezaji huo tofauti na hivi sasa.


Alisema ili bandari hiyo iingie katika upinzaniwa kiutendaji lazima iwe na uwezo wa kuwa na vifaa vya kisasa vya upakuwaji wa mizigo,technolojia bora na mifumo inayosomana ili kuweza kupunguza muda wa meli kukaa nangani unaosababisha kuongezeka kwa gharama.


Jerry Slaa Mbunge wa Ukonga alisema upo upotoshaji mkubwa unaofanywa ili Serikali isifanikiwe katika malengo yake ambayo ni kuifanya bandari hiyo kuwa lango kuu la mapato ya Nchi.


Alisema Mkataba au makubaliano yanayoendelea ndio msingi wa kisheria wa ushirikiano baina Tanzania na Kampuni hiyo DP WORLD na wananchi wanapaswa kutambua kwamba hakuna mradi utakaoanza hadi mkataba wa awali ukamilike.


Kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu CCM Taifa, Mwenyekiti CCM Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman alisema wale wanaobeza jitihada za Serikali katika mikakati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake ni jambo ambalo halitakubalika na kupewa nafasi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI