Header Ads Widget

TANESCO RUVUMA YAFIKIA MAKUBALIANO YA PAMOJA NA WAFANYABIASHARA WA VYUMA CHAKAVU ILI KUILINDA MIUNDOMBINU ISIHARIBIWE

  

Kaimu meneja wa Tanesco Mkoani Ruvuma   Malibe Boniphace
ACP RAMIA MGANGA
Richard Damas,Afisa usalama usimamizi Kanda ya kusini

Na Amon Mtega,Ruvuma

SHIRIKA la umeme Tanesco  Mkoani Ruvuma limeweka makubaliano ya pamoja na wafanyabiashara wa vyuma chakavu Mkoani humo katika suala zima la kulinda miundombinu mbalimbali iliowekwa na  Serikali kwa maendeleo ya Wananchi  ikiwemo ya Umeme ili isiharibiwe.


Makubaliano hayo yamefanyika kwenye  kikao cha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wa vyuma chakavu toka Wilaya zote za mkoa huo wakiwemo na Viongozi wa kamati ya ulinzi Mkoani huo ambacho kimejadili  juu ya mkakati wa kupambana na hujuma za miundombinu ya Umeme Mkoani Ruvuma.

 

 Akizungumza kwenye kikao hicho kaimu meneja wa Tanesco Mkoani Ruvuma mhandisi Malibe Boniphace amesema kuwa wameamua kufanya kikao hicho na kuwashilikisha wadau hao baada ya kubaini uwepo wa uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Tanesco ambayo imekuwa ikisababisha hasara kwa Serikali .


 Boniphace akizungumzia suala la miundombinu ya Umeme amesema kuwa wamekuwa wakikata nyaya za umeme , vyuma ambapo wateja wakubwa wa vifaa hivyo ni baadhi ya wanunuzi wa vyuma chakavu .


 Amesema kuwa kufuatia kikao hicho kutasaidia kushilikiana kuwafichua wahalifu ambao wamekuwa wakiiharibu miundombinu hiyo na kuwafanya baadhi ya Wananchi kukosa huduma za Umeme pamoja na kuisababishia hasara Serikali.


 Kwa upande wake mkuu wa Oparesheni Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Ramia Mganga amesema kuwa jeshi la Polisi lipo imara kupambana na wahalifu wa miundombinu hiyo kwa kuwasaka kila sehemu patakapo kuwa kumefanyika uharifu .


Kamishina msaidizi Mganga  ambaye amemwakilisha kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa Ruvuma ACP Marko Chiliya amesema kuwa baadhi ya wahalifu wa miundombinu ya Umeme ,Maji na ya barabara wameweza kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.


Amesema kuwa kuanzia sasa makubaliano yaliofikiwa na wafanyabiashara wa vyuma chakavu itasaidia kupunguza wimbi la wahalifu hao kwa kuwa wote watakuwa walinzi wa miundombinu hiyo.


Naye Afisa usalama usimamizi kanda ya kusini Richard Damas amesema kuwa vikao hivyo vitafanyika Nchi nzima kwa kuwa Serikali karibu kila mkoa kuna miradi mbalimbali  inafanyika ikiwemo ya Tanesco .


 Damas amesema kuwa kama wanunuzi wa vyuma chakavu wakipatiwa Elimu na kukaa  vikao vya pamoja miundombinu  mbalimbali ikiwemo ya Umeme haitaharibiwa kwa kuwa wote watakuwa sehemu ya walinzi wa miundombinu hiyo.


 Naye mmoja wa washiriki wa kikao hicho ,Kadoda Mbalale ambaye pia ni mfanyabiashara wa vyuma chakavu amesema kuwa kupitia kikao hicho wamepata uelewa juu ya kujiepusha kununua vyuma chakavu vinavyotokana na miundombinu ya Serikali.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI