Header Ads Widget

CCM BAGAMOYO WAUNGA MKONO UWEKEZAJI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.


Wilaya ya Bagamoyo imesema inamuunga mkono Mheshimiwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan kuhusu uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kwani ni uwekezaji mkubwa ambao ni kwa masilahi na Maendeleo ya Taifa letu.


Hayo yamesemwa na Mbunge Viti maalumu mkoa wa Pwani Subira Mgalu wakati akizungumza na Wanwnchi kwenye uzinduzi wa jiwe la msingi namba 4 la CCM Magulumatali katika Kata ya Talawanda ambapo mbio za Bendera ya CCM zilifika Kijijini hapo.

Subira amesema uwekezaji huo wa Bandari ya Dar es salaam unatarajia kulikusanyia taifa trioni 26.7 kutokana na ushuru wa forodha ifikapo mwaka 2032/2033 ambayo itasaidia nchi  kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo ya bajeti ya nchi yetu.


"Sisi wanabagamoyo tunatoa salamu kwa wanaondelea  kumbeza Mheshimiwa Rais sisi hatupo pamoja nao na wasikanyage kabisa Bagamoyo  na kwakuwa Sasa kupitia kampeni hii ya mbio za Bendera Chama kinaimarika sana wahesabu huku hawapati kitu kuanzia Uchaguzi wa 2024 hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kura kwa CCM ni za kishindo" Amesema Subira.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI