Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP,Moshi.
ZIMESALIA takribani siku tano ili kufikia tarehe 15.7.2023 ambapo umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)Moshi Vijijini wataendesha kikao chake cha baraza kwa mujibu wa kanuni na taratibu.
Kwa mujibu wa taarifa kwenda kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo julai 10.2023 na mwenyekiti wa umoja huo wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima ni kuwa kikao hicho cha baraza kitafanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini julai 15.2023.
'Niseme tu jambo kinaendelea Moshi Vijijini hakuna kupoa siku zinahesabika hivi sasa na wajumbe wake mkao tayari kwa tukio hili'imeeleza taarifa hiyo.
Aidha amesema kuwa maandalizi yote muhimu tayari yameshakamilika ikiwa ni pamoja na eneo la kufanya kikao hicho lakini pia kutaarifu wajumbe kama taratibu zinavyoelekeza
'Ninachotaka kusema hapa ni kuwa mambo ya msingi yameshakamilika na wajumbe wajitokeze kwa wingi katika baraza letu hili muhimu kwa ustawi wetu lakini na chama kwa ujumla wake'amesema
'Kama mwenyekiti nitumie fursa hii adimu kuwakaribisha wajumbe hawa katika mkutano huo na utakumbuka sisi ndio jeuri ya chama na alipo mama vijana tupo'anasema
Estomihi Urio ambaye amewahi kuwa kiongozi wa UVCCM miaka ya tisini amesema baraza hilo lina nguvu katika chama na kuwa limekutwa likitumika.kuwaandaa viongozi
'Ukiwa mjumbe wa baraza la UVCCM hiyo ni njia mojawapo katika kuwaandaa viongozi wakubwa serikalini lakini pia ndani ya chama'amesema
Naye Jackson Mori mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi kata ya Kilema Kusini anasema mabaraza haya ya vijana yana tafsiri nzuri kwani ndio hutumika kuwaandaa viongozi na ili uweze kiongozi Bora ni vyema kupitia katika hatua hiyo muhimu katika chama.
0 Comments