Header Ads Widget

RAIS SAMIA MGENI RASMI KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma 


RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT  Julai 10, 2023


Hayo yamesemwa na Waziri wa Jeshi la Ulinzi na Kujenga Taifa Innocent Bashungwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu kilele Cha Maadhimisho hayo.


Bashungwa ametumia nafasi hiyo kuwaalika  viongozi wote wa serikali, taasisi mbalimbali za Umma na binafsi , watumishi, Wananchi wa mkoa wa Dodoma na watanzania kwa ujumla  kujitokeza kwa wingi kuhudhuria siku ya kilele cha Maadhimisho hayo.


" Napenda kuwashukuru JKT kwa maandalizi ya Maadhimisho haya wadhamini na wote wanaoshirikiana na sisi katika maandalizi ya Julai 10 ya Miaka 60 ya JKT, " 


Na kuongeza" kwa namna ya pekee nishukuru uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa uratibu unaoendelea  katika kufanikisha Maadhimisho haya ya kihistoria," Amesema Waziri Bashungwa


Sambamba na hilo amesema kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT,kimetanguliwa na shughuli Mbalimbali ikiwa ni  pamoja na JKT Marathon 2023 iliyofanyika Juni 25 .


"Hii ni Marathon ya kwanza kuandaliwa na JKT tangu kuanzishwa kwake na ilifana Sana ,"

amesema  Waziri Bashungwa.


Pia Amesema Julai 1,2023 Makamu wa Rais , Dkt Philip Mpango alifanya uzinduzi wa Mnara wa Kumbukumbu katika makao makuu ya JKT (Chamwino Dodoma) na Kufungua maonesho ya bidhaa  ambayo yanaendelea hadi sasa  viwanja vya Medeli East Mkabala na SUMAJKT House.


"Huduma za kijamii Kama kutembelea  Hospitali ya Uhuru uliopo wilayani Chamwino pamoja na vituo vya kulelea  Watoto wenye uhitaji zimefanyika ," Amesema Waziri huyo.


Hata hivyo Waziri huyo ameendelea kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwani JKT pamoja na majukumu ya malezi lakini pia  wamekuwa wakiibua vipaji ambapo katika siku hiyo wananchi wataweza kushuhudia vipaji mbalimbali.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI