Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MAKAMU wa Rais Dkt,Philip Mpango amewataka wananchi kufika kwenye maonesha ya wiki ya kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuweza kujifunza na kunufaika na elimu inayotolewa na Jeshi hilo.
Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Suma JKT mjini Dodoma kuanzia Julai 1 Hadi 9 ambapo shughuli mbalimbali zinaendelea katika maonesho hayo
Dkt, Mpango amesema kufuatia maonesho hayo ya JKT viongozi wote hasa wakuu wa mikoa hawanabudi kufika na kujifunza elimu yote inayotolewa .
Pia mewataka Wananchi mikoa yote kujitokeze Kwa wingi katika wiki ya maonesha kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa ili kupata elimu na ufahamu juu shughuli za JKT
Aidha Dkt Mpango ametoa rai kwa JKT kupitia maadhimisho hayo kuendelee kujitanua Kwa kujitangaza na kuendeleza ushirikiano baina yao na Wananchi .
" Kupitia maonesha haya na uwepo wa wadau wengine niwazi kuwa itaifanya JKT kujipima katika ushindani wa utengenezaji wa bidhaa," amesema
Na kuongeza Kusema "Katika kutekeleza dhina yenu ya kuwafundisha vijana ujuzi,na ukakamavu muendelee kutilia mkazo katika suala zima la ulinzi wa Mazingira ni lazima kuwekeza nguvu katika vijana juu ya kutunza Mazingira na ongezeni bidii kwenye kupanda miti pia kufanya usafi kwenye kambi zetu," Amesema Dkt Mpango
Hata hivyo ameitaka JKT kuongeza matumizi ya Tekinologia katika kazi zao kwani zama za Sasa siyo zama za kutumia misuri na badala yake wawatambue wataalam wenye ubunifu Kwa kuwapatia tuzo.
" Pia niwaombe ongezeni msukumo katika kuibua vipaji kwenye michezo na nitoe pongeze Kwa timu zetu za Jeshi ambazo zinafanya vizuri katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa tangu kuanzishwa Kwa JKT limetimiza majukumu yake ya Msingi katika kuleta Umoja wa Vijana.
Aidha JKT inaendeleza shughuli za uzalishaji mali kupitia Shirika la SUMAJKT Kwa kutoa huduma mbalimbali,SUMAJKT toka kuanzishwa kwake limefanikiwa kushiriki Katika kuongeza ajira hapa nchini.
"Tunapoelekea kilele Cha maadhimisho ya JKT JKT imejipanga kutoa elimu ya kilimo Kwa Wananchi watakaotembelea maeneo ya maonesha halidhalika kutakuwepo na wanyama ambao ni rafiki katika maeneo haya"Amesema Mabele
Aidha ameongeza kuwa kutakuwepo na mabonanza ya mpira wa miguu,mpira wa pete pia kutakuwepo na shughuli mbalimbali kama kuwatembelea watu wenye mahitaji muhimu na kuchangia damu.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amesema kuwa kupitia kampuni ya SUMAJKT imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ikulu ya Chamwino.
Pia Wizara itaendelea kuiinjengea uwezo JKT katika kutimiza majukumu yake kupitia kampuni ya SUMAJKT
Mwisho
0 Comments