Header Ads Widget

MEYA AZICHAPA 'KAVU KAVU '

 Na Mwandishi Wetu MATUKIODAIMA MOSHI.


Huenda ni jambo ambalo lisilowezw kusahaulika katika historia ya manspaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo hii leo julai 13.2023 mstahiki meya Zubery Kidumo na diwani wa mji mpya Abuu Shayo wamekunjana mashati 

Naamini kila msomaji anataka kujua ilikuwaje ila picha halisi ni pale diwani huyo Abuu Shayo alipohoji baadhi ya matumizi ya fedha ambazo kimsingi haziendani na thamani ya kile kilichofanyika.

'Nimemuuliza mstahiki meya kuhusu matumizi ya fedha ikiwemo hizi zinazotumika kujenga uzio katika ofisi ya mkurugenzi kuwa mbona thamani ya hela haiendani na kazi inayofanyika'amesema

Kwa mujibu wa diwani huyo pia amehoji namna ya ujenzi holela unaoendelea katikati ya mji(CBD)ambapo kuna tuhuma za ofisi ya mstahiki meya kupokea rushwa kutoa vibali kinyemela.

'Mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi mimi nashangaa ila nilipouliza ndipo meya akatoka kwenye kiti chake na kunifuata nilipokuwa nimekaa ila ikabidi na mimi nijihami ila tumeshikana kiukweli'anasema

Anasema tatizo lililopo ni kuwa meya huyo hataki kuambiwa ukweli wala kushauriwa na leo katika kikao hicho cha kamati ya fedha kila akiulizwa kitu anakuwa na majibu yasiyo na mashiko.

Zuberi Kidumo ambaye ni mstahiki meya wa manspaa ya Moshi alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya tukio hilo alikana kutoka japo waliokuwa wanamzunguka walikuwa wakimpa pole kwa kadhia iliyojitokeza.

'Hakuna jambo lolote labda kama Kuna habari mpya tuongee na hivi vikao ujue ni vya ndani sasa nenda Kwa hiyo aliyekupa taarifa hizo'anaeleza Zuberi ambaye pia ni diwani wa kata ya NJORO.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI