Na,Jusline Marco:Arusha
Wenyeviti wa bodi za wakurugenzi , Wakurugenzi watendaji na Wataalamu wa Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa masuala ya Nishati Afrika Mashariki EREA kutoka Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na Tanzania wamekutana jijini Arusha kufanya tathmini na mipango kwa mwaka wa fedha 2023/24 kuhusiana na shughuli zake za kiutendaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt.James Andilile amesema kikao hicho ambacho kinahusisha takribani nchi 5 kwa madhumuni ya kuweka uwiano wa masuala ya udhibiti kisheria,kikanuni wa kikanda ili kuchochea uwekezaji katika sekta za Nishati kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa jamii.
Aidha Dkt.Andilile amesema Umoja huo umekuwa ukikutana mara mbili kwa mwaka ambapo amesema kwa mwaka huu ambao nchi ya Tanzania wakiwa wenyekiti wa Umoja huo chini ya Prof.Marck Mwandosiya kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa EREA,Tanzania imeweza kupata mafanikio katika mambo 3 ikiweko ukamilishaji wa usajiri wa EREA kupitia mamlaka zilizopo nchini.
Dkt.Andilile ameongeza kuwa mafanikio mengine ni upataji wa ardhi ya hekari 5 katika Mkoani Arusha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kudumu za Umoja huo pamoja na chuo ambacho kitakuwa kikitoa mafunzo kwa wadhibiti katika Kanda ya Afrika Mashariki pamoja na kuwezesha kuanza kwa utoaji wa mafunzo ya kiudhibiti kwa watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wataalamu kutoka Tanzania.
Ameongeza kuwa kikao hicho kitatoa fursa kwa wenyeviti hao kufanya maamuzi ya utekelezaji katika mwaka wa fedha 2023/24 ambapo amesema pamoja na uwepo wa ofisi hiyo nchi itaweza kunufaika kutokana na uwepo wa watu ambao watafika kupatiwa mafunzo na kutoa fedha sambamba na kutolewa kwa ajira.
Akizungumzia upandaji wa bei ya mafuta Dkt.Andilile amesema nchi ya Tanzania ndiyo nchi ambayo bei ya mafuta ipo chini ikilinganisha na nchi nyingine kwani suala hilo ni suala la kiuongozi na kimkakati ambalo serikali imejiwekea kwani masuala ya mafuta ni uchumi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ameupongeza Umoja huo kwa kuunda uwezeshaji wa kati wa kuboresha viwanda na miundombinu ya Nishati katika ukanda wa jumuiya ya Afrika mashariki .
0 Comments