Na Ibrahim Kunoga, Tanga.
Kutokana na shule ya msingi funguni iliyopo Wilayani pangani kukabiliana na adha ya uhaba wa matundu ya vyoo, mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah amekabidhi mradi wa vyoo kwa uongozi wa shule hiyo na vianze kutumika rasmi baada ya kuwa ujenzi wake umekamilika asilimia 100
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ziara yake ya twende na samia ya kijiji kwa kijiji ambapo amewashukuru na kuwapongeza mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga,Tanga Uwasa kwa kukamilisha utekelezaji wa mradi huo ambao unaenda kuondoa changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi kwenye shule hiyo.
"Niwapongeze Tanga Uwasa kwa kukamilisha utekelezaji wa mradi huu na hii ni hatua kubwa sana na muhimu kwetu na niwambie tusimamie na kutumia vyema miundombinu yetu;Alibainisha Mkuu wa wilaya Zainabu.
Geoffrey Hilly ambae ni mkurugenzi mtendaji wa Tanga Uwasa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, ameeleza kuwa hiyo ni sehemu tu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kutibu tope, ba kinyesi mjini pangani.
Mkurugenzi Hilly amesema kwa kuwa ujenzi wa vyoo katika shule hiyo umekamilika kwa asilimia 100 na kunauhitaji anaomba akabidhi miundombinu kwa uongozi wa shule na uanze kutumika na wanafunzi, wakati wakiendelea na ukamilishaji wa sehemu nyengine ya miradi iliyobaki
Aliiendelea kwa kusema kuwa mradi huo unasehemu kuu tatu zinazohusisha ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kuchakata maji taka eneo la kumba mtoni ambapo kazi yake imefikia asilimia 92 ujenzi wa vyoo katika maeneo matatu ikiwemo, shule ya msingi na sekondari funguni, kituo cha mabasi mjini pangani, na manunuzi ya magari mawili ya usimamizi wa mradi na gari ya kunyonya na kusafirisha maji taka ikiwa mradi huo unatekelezwa na mkandarasi M/S Pertels company ltd kwa gharama ya shilingi 998,545,461.56 na unatarajiwa kukamilika septemba 2023.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo mwalimu Flora. Amefurahishwa kwa uwepo wa miundombinu hiyo ambayo inaenda kusaidia wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wanapitia changamoto kwa muda mrefu.
0 Comments