Na Gabriel Kilamlya-Matukio DaimaAPP, NJOMBE.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe.Edwin Enosy Swalle amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya elimu hapa nchini ikiwemo katika jimbo lake ili kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa katika nchi hii aweze kupata Haki ya msingi ya elimu.
Mbunge Swalle amezungumza hayo alipotembelea mradi wa shule ya sekondary iliyopo kata ya Ikondo katika jimbo la Lupembe ambapo amesema kuwa wanafunzi wa sekondari katika kata hiyo wamekuwa wakifuata elimu umbali mrefu katika kata jirani ya Ukalawa hivyo serikali kwa kulijua hilo imetoa fedha ili kujenga shule mpya na yakisasa katika kata hiyo.
Pichani: Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe.Edwin Swalle.
Aidha Mbunge huyo amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha miundo mbinu ya elimu ili watoto wa kata hiyo waweze kupata haki yao ya elimu na hivyo baadaye kupata wasomi wengi zaidi hapa nchini wakitokea katika jimbo la Lupembe.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ikondo Milius Lupenza amesema kuwa Shule hiyo imeanza Kuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hiyo kwani hapo awali watoto wengi walikuwa wakitembea umbali wa Km 20 kufuata huduma ya elimu na hivyo kupelekea wengine kuwa watoro lakini mara baada ya serikali kujenga shule ndani ya kata hiyo changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu imeondoka kabisa.
Picha: Shule mpya ya Ikondo Sekondari Lupembe Njombe.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ikondo Sekondari Mekraud Kyando amesema kuwa tangu shule hiyo ianze taaluma katika shule imeimarika huku wanafunzi wa wakimshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo ya kisasa katika kata hiyo.
0 Comments