Header Ads Widget

ZUENA BUSHIRI MBUNGE ANAYEPAMBANA KUHAKIKISHA MATATIZO YA WANANCHI WA MKOA WA KILIMANJARO YANAPATIWA UFUMBUZI.

 


NA WILLIUM PAUL.

MBUNGE wa Viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameendelea kupambana kuhakikisha tatizo la ubovu wa barabara katika mkoa wa Kilimanjaro linapatiwa ufumbuzi wa kudumu na wananchi wanaondokana na adha hiyo.


Mbunge huyo leo amehoji Bungeni ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Makanya - Ruvu ambayo inakwenda katika machimbo ya Jipsam.


Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya alisema kuwa, barabara hiyo ni ya kimkakati ambayo inaenda katika maeneo maalum ya kiuchumi.


Mhandisi Kasekenya aliendelea kudai kuwa, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.


Hatua hiyo ya Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri kupigania maslahi ya wananchi Bungeni imepokelewa kwa furaha kubwa ambapo wamempongeza Mbunge huyo kwa juhudi anazofanya.



Asha Ramadhani mkazi wa Majengo alisema kuwa, Mbunge Zuena amekuwa akifanya kazi ambayo wamemtuma kwenda kuwapigania na kuwatetea maslahi yao.


"Kwa sasa wanakilimanjaro tunatembea kifua mbele kwa kuwapata wabunge ambao wamekuwa wakitupigania na hili Zuena anatuonyesha kwa vitendo tunaona na kusikia yale anayoyafanya Bungeni" alisema Asha.


Naye Mwajuma Shabani mkazi wa Pasua alomuomba Mbunge huyo kutokukata tamaa katika kupambania maslahi ya wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na kudai kuwa wataendelea kumuunga mkono katika juhudi zake hizo.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI