Na Fadhili Abdallah,Kigoma
HALI si shwari ndani ya Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kufuatia kusimamishwa uongozi kwa aliyekuwa Katibu wa chama hicho kanda ya magharibi Ismail Kangeta kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mikutano ya kampeni ya katiba mpya iliyoendeshwa na chama hicho mkoani Kigoma Mwezi uliopita.
Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi CHADEMA, Gaston Garubindi akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma alisema kuwa kufuatia tuhuma hizo kamati ya ya utendaji kanda ya Magharibi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imemsimamisha uongozi katibu huyo ili kupisha uchunguzi na hatua nyingine za kinidhamu.
kamati hiyo ya utendaji ya kanda imetoa mapendekezo yake kwa kamati kuu ya Taifa ya CHADEMA kumuomba imchukulie hatua zaidi za kinidhamu.
Mwenyekiti huyo wa kanda alisema kuwa kusimamishwa kwa katibu huyo wa CHADEMA mkoa kigoma ni hatua ya awali katika kuelekea
kuchukua hatua zaidi kwa kiongozi huyo na tayari kamati hiyo ya utendaji ya kanda imetoa mapendekezo yake kwa katibu kuu ya Taifa ya CHADEMA kumuomba imchukulie hatua zaidi za kinidhamu.
Kufuatia hali hiyo alisema kuwa Kamati ya utendaji kanda imemteua Afisa wa fedha na Oganaizasheni Paul Jinery kukaimu nafasi ya katibu wa CHADEMA kanda ya Magharibi hadi hapo utaratibu mwingine wa kujazwa kwa nafasi hiyo utakapofanywa.
Mwenyekiti huyo wa kanda ya Magharibi CHADEMA alisema kuwa pamoja na ubadhirifu huo wa fedha uliuofanywa na kiongozi huyo mikutano kwa ajili ya kampeni ya Katiba Mpya iliyofanywa na Mwenyekiti,Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu ambao waligawana makundi mawili ilifanyika na kuwa na mafanikio makubwa kulinagana na malengo yaliyowekwa kwenye kampeni hiyo.
Mwisho
0 Comments