Header Ads Widget

WAZIRI UMMY AKUTANA NA RAIS NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HJFMRI



Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Juni 20, 2023 amekutana na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Jackson Foundation For Medical Research International (HJFMRI) Maj. Gen. Dkt. Joseph Caravalho na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Afya ikiwemo utolewaji wa huduma za VVU nchini.


Katika kikao hicho Waziri Ummy amemshuruku Mkurugenzi huyo kwa msaada ambao umekuwa ukitolewa kwa Timu za Usimamizi wa Afya za Mikoa na Halmashauri katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kupitia ruzuku ya moja kwa moja, maendeleo ya miundombinu na utoaji wa huduma za VVU.


Aidha, Waziri Ummy amesema HJFMRI imekuwa mshirika wa kimkakati katika kutoa takwimu muhimu, kupitia shughuli zake za utafiti wa ndani ya nchi ambapo Matokeo ya utafiti yamekuwa muhimu kufahamisha sera mbalimbali za kitaifa zinazohusiana na VVU na UKIMWI. 


Vile vile katika kuimarisha na kujenga uwezo kwa taasisi zetu za utafiti hususan NIMR na watoa huduma za Afya.


“Ningependa kutoa shukrani zangu kwa shirika lako kwa kuendelea kuunga mkono mpango wa DREAMS unaolenga kuzuia Maambukizi ya VVU yasiongezeke kwa Watanzania”. Amesema Waziri Ummy


Lakini pia, Waziri Ummy ametoa maombi mawili kwa Rais na Mkurugenzi huyo wa HJFMRI ikiwemo la kusaidia Watoa huduma ngazi ya jamii (CHW) kwa kuajiri na kutoa elimu juu ya VVU, Magonjwa Yasiyoambukiza, Magonjwa Yakuambukiza pamoja na Lishe.


Pili, kuwajengea uwezo viongozi wa Taasisi zetu pamoja na kusaidia kuajiri wataalamu wa ubingwa bobezi ili kupata wataalamu wengi zaidi ambao wanaweza kutoa huduma za Ubingwa Bobezi nchini. 


Kwa upande wake Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Jackson Foundation For Medical Research International (HJFMRI) Maj. Gen. Dkt. Joseph Caravalho amemshukuru Waziri Ummy kwa kumkaribisha na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Shirika hilo. 


“Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Afya kwa kutoa takwimu sahihi za VVU, pia tutaendelea kutoa Elimu zaidi juu ya Kujikinga na VVU kwa Watanzania”. Amesema Maj. Gen. Dkt. Caravalho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI