Header Ads Widget

WAKULIMA WAPATIWE MBEGU BORA ITAKAYOKUWA MKOMBOZI KWENYE SOKO

 


 


 Na Matukio daima,Mbeya  


SHIRIKA lisilo la kiserikali la wadau wa kilimo (ANSAF,) limeweka mikakati ya kuboresha kilimo cha zao la kahawa  kwa wakulima ili kuongeza tija ya uzalishaji na kufikia malengo.


Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo ,Honest Mseri amesema leo kwamba wamelazimika kufanya hivyo kutokana na uzalishaji kuwa   mdogo .


Mkutano huo  wa siku moja ulioshirikisha  wadau , maafisa kilimo wa serikali , wafanyabiashara , sekta binafsi pamoja  na wakulima  kutoka mikoa mitatu ambayo ni , Mbeya, Songwe na Ruvuma .


Amesema  kuwa kutokana na zao la kahawa kuwa kongwe  hapa  nchini  ni wakati sasa wa kuboresha mifumo ya upatikanaji wa miche bora ambayo italeta tija kubwa katika uzalishaji na mikoa husika kufanya vizuri zaidi kwenye kilimo hicho.


“ Siku zote wakulima wamekuwa wakiangalia zao ambalo linawapatia kipato hivyo ili kuweza kuwavutia  ni lazima kuwa na mbegu bora ambayo itakuwa msaada kwa mkulima .”amesema.


Amesema kuwa wastani wa  asilimia 90 ya kahawa inasafirishwa kwenda nje ya nchi na ndio sababu kubwa ya kuwakutanisha wadau ili  kutengeneza soko la ndani  na kuvutia wanunuzi wengi ili kuboresha kipato cha wakulima.


Amesema kuwa lengo kubwa ni kuona zao la kahawa lina fursa kubwa ya kuendelea kutoa fursa za ajira hususan  maeneo mengi yanayolima yanakuwa na  Maendeleo makubwa ukilinganisha na maeneo yasiyolima kahawa ili kuongeza kushawishi kuzalisha kwa tija kubwa..



Kwa upande wake ,Labeli Ulomi ni Meneja uzalishaji kampuni ya ukoboaji Kahawa Mbimba iliyopo mkoani Ruvuma  amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma una ardhi kubwa ambayo inafaa kwa kilimo ambayo bado haijatumika na yenye rutuba na halmashauri ya Mbinga pekee ina kiasi cha hekta 25,000  ambazo zingeweza kulima kahawa lakini hazijaweza kutumika kwa ajili ya kilimo cha kahawa hivyo ni ni fursa kubwa kwa kilimo cha kahawa  ikifuatiwa na Nyasa ambayo ina hekta zinazozidi 6,000 ambazo hazijatumika kwa ajili ya kilimo cha kahawa .


Dismas Pangalasi ni Meneja wa programu za utafiti  wa zao la Kahawa Kanda ya Mbeya ,amesema kuwa jukumu lao ni kutoa mafunzo kwa wakulima pamoja na kuzalisha miche bora ya kahawa  na kwamba kwa mwaka 2022/2023 wameweza kuwafikia wakulima  7,640 katika mkoa wa Mbeya na Songwe kwa wilaya nne na  kutoa mafunzo ya ,mabadiliko ya tabia nchi  kwa wakulima 9,530 .

 


Alitaja   fursa kubwa  wanaweza kuzipata wakulima ni kutoka  Taasisi ya utafiti wa kahawa ambayo ipo kwenye maeneo yao ,pia wana aina 13 bora za kahawa ambazo zinazalishwa kituo cha utafiti Tacri Mbimba na kuwa aina hizo za mbegu hazishambuliwi na wadudu.

 


Akizungumza na majira mmoja wa wakulima wa kilimo cha Kahawa , Jeremiah Mwaje amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akijishughulisha na kilimo cha Kahawa ambacho mwanzo alikuwa akipata kahawa kwa wingi lakini hivi sasa changamoto ipo kwenye soko na ubora wa mbegu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS