Na Matukio daima,Dodoma
NAIBU waziri wa Maji mhandisi ,Maryprisca Mahundi (MB)ameiagiza bodi mpya ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma pamoja na menejimenti ya mamlaka hiyo (DUWASA)kusimamia mikakati na kuendelea kupunguza kiasi cha upotevu wa maji kufikia chini ya asilimia 20 kinachokubalika kimataifa.
Pia Mhandisi Mahundi amesema bodi hiyo mpya ina mamlaka ya kusimamia ipasavyo miradi yote ya maji pamoja na kuhakikisha uwepo wa thamani ya fedha (value for money) katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhandisi Mahundi amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa bodi ya tisa pamoja na uzinduzi wa mradi wa maji wa Ntyuka-Chimalaa (Dodoma).
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema bodi hiyo mpya kwa kushirikiana na menejimenti ya DUWASA kuendelea kuwahudumia ipasavyo wakazi wa Dodoma huku miradi ya muda mfup ikiendelea kutekelezwa ili kupunguza changamoto ya maji wakati serikali ikijipanga kutekeleza miradi mikubwa ya kumaliza tatizo la maji kwa miaka 30 – 50 ijayo.
Aidha Naibu waziri wa maji huyo ambaye pia mi Mbunge wa vitimaalum mkoa Mbeya amesema bodi hiyo mpya pia ina wajibu wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji ili upatikanaji wa huduma ya maji kufikia asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025 kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyo elekeza
Uzinduzi huo umehudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Dodoma, Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Wajumbe wa Bodi ya waliomaliza muda wao-DUWASA, wajumbe wa Bodi mpya-Duwasa pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Maji.
0 Comments