Header Ads Widget

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA MICHEZO KUINUA PATO LA TAIFA

 






MRATIBU wa ligi ya mpira Mbweni Super Cup na mwenyekiti wa CCM kata ya Mbweni  Abdulkhadir Mgheni amewataka vijana kutumia fursa kupitia michezo hususani ligi mbalimbali zinazoanzishwa ikiwemo ligi inayoendelea katika kata hiyo ili kujipatia ajira za uhakika na kuongeza pato la Taifa


Mwenyekiti huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari baada ya uzinduzi wa ligi hiyo Mbweni katika uwanja wa Mbuyuni


Amesema uwepo wa ligi hiyo kutachochea zaidi vijana wenye vipaji kuweza kujitokeza na kusajiliwa na timu kubwa ambazo zinatumia pesa nyingi kununua wachezaji wa kigeni na kuwaacha vijana wakikaa vijiweni bila mafanikio


Abdulkadir ametumia fursa hiyo kumshukuru Raisi wa awamu ya Sita Dokta Samia Suluhu Hassani kwa kuchochea vijana wa kitanzania kujiingiza katika michezo na kuitumia kama njia ya kupata ajira ya uhakika kulingana na soko lilivyo katika dunia 


Naye Diwani wa kata hiyo Singo Mtambalike ameishukuru serikali kwa kuwapatia vijana viwanja vya uhakika ukilinganisha na awali ambapo vijana walikosa maeneo muhimu ya kuchezea, "wanamichezo pamoja na wadau karibuni Mbweni, kupitia michezo hii mtajionea fursa mbalimbali kupitia ligi hii ya Mbweni Super Cup" alisema


Akizindua ligi hiyo Jana Askofu Josephat Gwajima amesema vijana wa kata ya kawe wana vipaji vya kutosha, na kuitaka timu za ligi kuu ikiwemo KMC Kufika kuangalia vijana ili waweze kunufaika, askofu Gwajima amesema nidhamu na malengo ndio silaha kwa wanamichezo wote na kuwataka kucheza kwa nidhamu 


Mshindi wa kwanza atajipatia shilingi 300,000 pamoja na zawadi zingine kwa washindi na wachezaji bora, mfungaji bora na timu yenye nidhamu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI