NA WILLIUM PAUL,
SERIKALI inategemea kuanza ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (Veta) katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ili kuwasaidia vijana kupata taaluma za fani mbalimbali hali ambayo itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri kuhoji Bungeni je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa chuo cha Veta wilayani Rombo kwa kuwa Halmashauri imeshatoa eneo na wataalam wa ardhi walishafanya uchambuzi na kuona eneo hilo linafaa.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga alisema kuwa, katika ujenzi wa vyuo 64 vya wilaya zilizobaki Rombo ni miongoni wa wilaya ambayo inaenda kujengewa.
Naibu Waziri Kipanga alidai kuwa, kazi imeshaanza ambapo wameanza na utaalam wa ramani pamoja na kufanya tathimini ya adhari za kimazingira.
Alisema kuwa, pia wameshatambua eneo na shughuli za ujenzi wa chuo hicho zimeanza katika mwaka fedha.
Ujenzi wa chuo hicho utafungua milango ya fursa kwa vijana ambao hawachaguliwi kuendelea na Elimu ya juu kujiunga katika chuo hicho na kupata utaalam wa fani mbalimbali na kujiinua kiuchumi.
Mwisho..
0 Comments