Na Teddy Kilanga, Matukio Daima App
KANISA katoliki jijini Arusha liko mbioni kurejesha milioni 50 ilizotenga kwa ajili ya kuwakopesha vijana bila riba ili wajiinue kiuchumi kwa kile kilichoelezwa kuwa wanapuuza vigezo rahisi vilivyowekwa ili kuzipata fedha hizo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha wanataaluma wakristo (CPT) jimbo kuu la Arusha Nicholaus Mlawa wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya chama hicho yenye lengo la kurejesha fadhila kwa jamii kupitia taaluma walizo nazo ambapo amesema kuwa vijana wengi wameshindwa kutumia fursa ya fedha hiyo.
Aidha amesema kuwa fedha hizo zimeletwa ili kuwasaidia vijana ambazo zinatolewa bila riba lengo ni kutengeneza mradi utakaowasaidia kuwanufaisha katika kujikwamua kiuchumi lakinibwameshindwa kutumia fursa ya fedha hizo na muda ukiiisha zitarufishwa zilipotoka.
"Vijana wengi wamekuwa hawana mwelekeo katika maisha kwa sababu ya kukosa muongozo kwa waliofanikiwa hivyo ni wajibu kwa wanataaluma kuwasaidia katika kutumia fursa mbalimbali,"alisema.
Awali mlezi wa chama hicho Gaspa Leo amehamasisha wananchi kushiriki maonyesho hayo kwani watapata fursa ya kupata elimu ya masuala ya bima, msaada wa kisheria, Tehama, ardhi, kilimo, mifugo, ufundi stadi na upimaji wa magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza.
Leo amesema ni wakati wa wanataaluma kurudisha kwa jamii kile walichokipata lakini changamoto ya vijana wengi kutumia fursa ya mikopo hiyo ni pamoja na kushindwa kuandaa mawazo ya kibiashara na kuyatetea namna watakapoendesha miradi yao ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.
"Vijana wengi wanahitaji kupewa bila muongozo wowote hali ambayo haiwezekani kwani ni lazima wawajibike katika jamii sambamba na kujishughulisha kiuchumi ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.
0 Comments