Header Ads Widget

NDEGE YA MIZIGO AINA YA BOENG 767-300F KUTUA LEO NCHINI

 



Jusline Marco;Arusha


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan hii leo anatarajia kupokea ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeng 767-300F tukio ambalo litafanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.


Akizungumza jijini Arusha na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Utalii ya Karibu KillFair, Meneja Mipango wa Mtandao na Usimamizi wa Mapato kutoka ATCL, Edward Nkwabi amesema kuwa ni miongoni mwa ndege mpya nne ambazo wanatarajia kuzipokea ndani ya mwaka huu.


Aidha Nkwabi amesema kuwa ujio wa ndege hizo kutaongeza safari za kimkakati katika ufunguaji wa soko la Afrika Magharibi kupitia safari za kwenda Lagos nchini Nigeria.


"Serikali inaendelea kuliboresha shirika ambapo kwa mwaka huu tunatarajia kupokea ndege zingine nne lakini pamoja na hiyo ndege ya mizigo tunataraji mwaka huu kundelea kupokea ndege mbili  ambao ni aina ya Boeng 737 MAX 9."Alisema Nkwabi


Ameongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kupakia abiria 184 ambazo zitaenda kuongeza nguvu kwenye safari  za kimkakati katika kufungua soko la Afrika Magharibi ambapo safari zitaanza za kwenda Lagos nchini Nigeria


Sambamba na hayo amesema pia wanaagazia kufungua safari ya Dubai ambayo imekuwa na mwamko mkubwa na uhitaji kutoka kwa wadau ikiwa ni kiliangalia soko la Afrika Kusini ambalo nila muhimu kutokana na watalii wengi ambao waliokuwa wanawapata kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania.


"Ukiangalia hasili ya utalii nchini kuna kutegemeana ambako kunatengeneza kuwa  a siku nyingi zaidi za watalii kuja kufanya utalii hapa nchini."Aliongeza Nkwabi Meneja Mipango wa Mtandao na Usimamizi wa Mapato kutoka ATCL, Edward Nkwabi 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS