Header Ads Widget

MVUTANO WA WAPI KIJENGWE CHUO KIKUU NJOMBE WAMALIZWA NA RCC

 

Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka
Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Kwa kauli Moja kikao Cha Kamati ya ushauri mkoa wa Njombe RCC kimeridhia Njombe mjini ndipo kitakapojengwa chuo kikuu Cha serikali cha mkoa na sio mahala pengine.


Hatua hiyo inakuja baada ya kuwapo kwa  mvutano wa muda mrefu wa wapi kitajengwa chuo hicho Kati ya mji wa Njombe na Makambako ambao waliwasilisha maombi kwenye mkoa Pindi serikali itakapoleta fedha Kama ambavyo Rais Samia alivyoahidi wakati wa ziara yake mkoani Njombe.


Wajumbe wa RCC mkoa wa Njombe wakiwemo Viongozi wa vyama vya siasa Lukule Mponji, Ally Mhagama na Rose Mayemba pamoja na  Wafanyabiashara waliowakilishwa na mwenyekiti wao Eliud Pangamawe wamesema historia ya maeneo ya ujenzi wa vyuo vikuu huanzia kwenye kitovu Cha Makao makuu na kwamba wanaona ni muhimu kujenga katikati ya mji wa Njombe.


Wabunge  wa majimbo ya mkoa wa Njombe Deo Mwanyika,Joseph Kamonga na  Deo Sanga ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe wamesema kwa kuwa wajumbe Wengi wametaka chuo kikuu kijengwe Njombe mjini nao hawawezi kupingana na hoja zao.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema waliandaa maeneo matatu tofauti katika Halmashauri hiyo Likiwemo la Uwemba,Ihalula na Jirani na Shule ya Sekondari Njombe[NJOSS]eneo ambalo limeridhiwa na wajumbe wengi kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Mkoa.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema kama mkoa utawasilisha maazimio ya kikao hicho katika ngazi zinazofuata kwani RCC ndio kikao chenye maamuzi ya mwisho kwa ngazi ya Mkoa.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI