Header Ads Widget

MSUKUMA AWATOA HOFU WA TANZANIA

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

MBUNGE wa Geita vijijini Joseph Musukuma amewataka watanzania kuunga mkono azimio la serikali kuingia na serikali ya Dubai katika ushirikiano wa Kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendekezaji na uboreshaji na utendaji kazi wa Bandari na kama kuna mapunguvu yatasimama kwenye mkataba.


Amesema kwa sasa kinachojadiliwa ni makubaliano ya nchi na nchi na hakuna aliyeuona mkataba huo.


Msukuma, ameyasema hayo leo Jijini hapa aliokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uvumi ulioshika kasi hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa bandari hiyo imeuzwa na wengine wakisema imekodishwa kwa mkataba wa miaka100.

 

Amesema maneno yanayoandikwa kwenye mitandao sio ya kweli kwani hata Rais Samia atastaafu na kuishia maisha kama wananchi wengine .


"Sio kweli Rais kwenda kusaini mkataba ambao hauna maslahi kwa Taifa hili labda yeye kama iwe akistaafu anahama Tanzania lakini hapana tusikatishane tamaa," Amesema Musukuma , 


Na kuongeza Kusema"Turudi  nyuma watanzania hakuna mkataba wa kimkakati ambao tumeufanya kwenye awamu zote bila kuwa na kelele na kelele hizi zinatengenezwa na watu wasioitakia mema nchi yetu,"amesema Msukuma.


Hata hivyo, ameseama hata kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati Rais Magufuli, alipotaka kuanza ujenzi wa bwawa la kufua umeme Rufiji wapo waliopiga kelele lakini serikali haikukatishwa tamaa.


“Wakati ule watu walipiga sana kelele kuliko hata hizi lakini Magufuli alijenga bwawa la Rufiji na hivi sasa bwawa hilo hilo watu wanaliombea kura wakati wa uchaguzi kwa wapiga kura wao”alisema Msukuma


Amesema Bandari ndio uwekezaji mkubwa na  bandari ya Dar es salaam imekuwa na tija kwa wafanyabiashara ndani na nje ya nchi.


"Tuache kudanganyana mimi nimefika Dubai nimejionea namna bandari za wenzetu zinavyofanya kazi, uwekezaji unaofanywa na serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia utasaidia sisi wafanyabiashara kutuondolea malalamiko ya kucheleweshewa kupata mizigo yetu kwenye bandari"amesema Musukuma


Amesema kuwa hali iliyopo sasa katika bandari kwenye upokeaji wa mizigo unachukua muda mrefu na inasababisha wafanyabiashara wengi kuagiza mizigo kupitia bandari nyingine ikiwemo bandari ya Mombasa.


"Rais ni taasisi siyo mtu mmoja ina watu wengi sio kwamba wanavyozungumza mitandaoni hakuna tafiti zilizofanyika, Ikulu imefanya utafiti na sisi wabunge baadhi tulienda kuona na kuona ni kuamini, na sio wanaozungumza mitandaoni wanauwezo mkubwa sana sio kweli unaweza ukawa na uwezo mkubwa wa kuzungumza mitandaoni lakini hujui mateso yaliyopo bandarini ukabaki tu kushinda mitandaoni, kujadili wenzio na kupiga vitu ambavyo huna uhakika navyo,"amesema Msukuma.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI