NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Chema Tarafa ya Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kutoa mahubiri yenye kupotosha jamii.
Mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Herman Magigita mwenye umri (60) mchungaji wa kanisa la NENO alikamtwa baada ya kutoa mahubiri ya kupotosha waumini wake wasiende Hospitali kupata matibabu pindi wanapougua badala yake wawapeleke katika kanisa hilo kwa ajili ya maombezi.
Kamanda wa Polisi Mkaoni hapa Wilbroard Mutafungwa ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamtwa baada ya Jeshi hilo kupata taarifa za uwepo wa mchungaji huyo anayetoa mahubiri ya kupotosha na kufanya shughuli za kanisa bila kuwa na kibali cha usajili kinyume na sheria.
"Tulipata taarifa kuwa kuna mtu anatoa mahubiri ya kupotosha jamii ambapo askari polisi walifika katika kanisa hilo na kufanikiwa kumkamata" Alisema Mtafungwa.
Mutafungwa ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yao.
0 Comments