Header Ads Widget

MBUNGE JOSEPH TADAYO ATOA VIFAA VYA MICHEZO KATA YA LANG'ATA



NA WILLIUM PAUL, MWANGA.


Katika kuhakikisha anakuza na kuendeleza vipaji vya michezo Wilayani Mwanga, Mbunge wa Jimbo hilo, Joseph Tadayo amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira kwa timu zote 6 zinazoshiriki ligi hiyo iliyo chini ya UVCCM Kata ya Lang'ata.



Akikabidhi vifaa kwa niaba ya Mbunge, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga Aisha Mfaume amewataka Wachezaji na Viongozi wa timu kutumia nafasi hii ya michezo kuungana na sio kuleta vurugu uwanjani



Aliendelea kusema amemwakilisha Mbunge ambapo yeye yupo kwenye majukumu mengine ya kikazi na kuwakabidhi vifaa hivi kwa niaba yake.



Ligi hiyo inayoshirikisha timu 6 ambapo timu 5 zinatoka Kata ya Lang'ata na timu moja inatoka Kata ya Mwanga,mshindi wa kwanza atapata laki moja na mshindi wa pili atapata mbuzi.



Wengine waliohudhuria ufunguzi wa ligi hiyo ambapo wamecheza ufunguzi  ni Lang'ata ndogo Vs Mwanga ni Katibu wa Vijana Wilaya, Katibu Hamasa Wilaya,  Diwani Kata ya Langata na Viongozi wa CCM Kata pamoja na UVCCM Kata na Matawi yote.



Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI