Header Ads Widget

MAOFISA WATENDAJI WALEVI NA WASUMBUFU KAZINI WAONYWA VIKALI NJOMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka

                                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Maofisa watendaji wa kata na makatibu tarafa mkoani Njombe wametakiwa kutumia taaluma zao kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo badala ya kuendekeza ulevi,uvivu na hata migogoro inayoweza kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka wakati akifunga mafunzo ya utendaji kazi ya siku mbili kwa maafisa hao yaliyofanyika chini ya ofisi ya Rais Tamisemi kupitia chuo cha Utumishi Hombolo kilichopo mkoani Dodoma.


Aidha Mtaka amesema licha ya kazi kubwa ya kutukuka inayofanywa na baadho ya maafisa hao lakini wapo ambao wanaendekeza ulevi,wizi,na kushindwa kukusanya mapato kama inavyostahili jambo ambalo halipaswa kufumbiwa macho kwa mtumishi wa umma.


Akizungumza kwa niaba ya Makatibu tarafa wa mkoa wa Njombe Katibu tarafa ya Lupalilo Augustino Ngailo amemshukura Rais kwa kuwaletea mafunzo hayo ambayo yamewapa molari mpya ya kwenda kutekeleza kwa weledi majukumu yao ya kuwatumikia watanzania.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala ofisi ya Rais Tamisemi John Cheyo amesema baada ya kuwapo kwa changamoto nyingi za utendaji kazi kwa maafisa watendaji hao zilizokuwa zikitokana na kukosekana kwa uelewa serikali ililazimika kuchukua hatua ya kuwapa mafunzo hayo.


Hata hivyo baadhi ya maafisa Watendaji hao akiwemo Daria Kilasi na Festo Mbakilwa wamekiri kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kwenda kuboresha utendaji kazi huku wakiwataka walevi kuachana na tabia hiyo inayoweza kukwamisha kazi.


Tayari mikoa minne imefikiwa katika utoaji mafunzo hayo kwa maafisa watendaji na maafisa tarafa kwa Tanzania Bara na mikoa 22 itafuata katika mwaka mpya wa fedha ujao.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI