Header Ads Widget

LINDI YAPOKEA MTAMBO WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA MAJI

 




 Na HADIJA OMARY _LINDI....



Mkuu wa mkoa wa Lindi Bi.Zainab Telack amepokea mtambo  wa uchimbaji wa visima ulionunuliwa kupitia fedha za uviko 19 ambao utakuwa unafanya kazi hiyo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.



Hatua hiyo inakuja katika hatua mbalimbali za Serikali kuendelea kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa maji na kufikia wastani wa asilimia 85 ya upatikanaji huduma hiyo Vijijini na asilimia 95 mijini  ifikapo 2025, 



Ghafla ya makabidhiano ya mitambo hiyo imefanyika leo june 5 2023 katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo na kuudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali 




Akizungumza wakati wa ghafla hiyo Telack  ametumia nafasi hiyo kuwataka wataalamu na wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini Ruwasa kuhakikisha wanaitunza ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma ya maji safi.



Alisema dhamira ya Rais samia iliouwa njema kwa kutumia fedha za Uviko 19 kupeleka katika uwekezaji mkubwa wa miradi ya maji ili kuwawezesha wananchi wake kukabiliana na changamoto hiyo hivyo ni vyema mitambo hiyo ikatunzwa ili itumike kwa muda mrefu.


Awali akisoma taarifa ya mtambo huo kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa   afisa usafirishaji   Yusuf Mtambo  amesema  mtambo huo unauwezo wa kuchimba kisima hadi mita 300 chini ya ardhi  na kuchimba visima sita kwa mwezi 




"Hii inamaana kwamba tunategemea kuchimba  visima  66 kwa mwaka kutegemea na upatikanaji wa rasilimali fedha , miundombinu ya eneo husika , hali ya hewa na hali ya mtambo  utakavyokuwa kwa kipindi hicho "



Kwa upande wake meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini Ruwasa Mkoa wa Lindi Mhandisi Muhibu Lubasa amesema kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji kwa mkoa huo ni asilimia 68.5 mjini na asilimia 71 vijijini.


Alisema kupokelewa kwa mitambo hiyo ni wazi kuwa   itakwenda kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji wa asilimia 85 kwa vijijini na 95 mijini kama ilani ya uchaguzi inayotaka kufikia 2025 kwani watakwenda kutafuta vyanzo vya maji na kwa visima vitakavyopata maji mengi watavitumia kusambaza maji vijijini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS