OR-TAMISEMI
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa, Mhe.Denis Londo ameshauri kuwepo na mpango wa pamoja shirikishi wa kupanga maeneo kwenye Miji ili kuondoa ugumu wa upatikanaji wa maeneo ya kujenga miundombinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART) miaka ijayo.
Mhe.Londo ameyasema hayo Juni 17, 2023 kwenye ziara ya kamati hiyo ilipotembelea DART kujionea maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya DART awamu ya tatu mkoani Dar es salaam. Mwenyekiti huyo amesema Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) wanapaswa kuongozwa kwenye mikakati ya kuwa na miundombinu katika Miji inayokua ili suala la ugumu huo lililojitokeza kwa Dar es salaam lisijirudie.
Amesema katika miaka 15 ya mradi huo makazi yanaendelea kukua na watu wanagawiwa viwanja bila kujali maeneo yatakayopitiwa na miundombinu ya mradi hapo baadae hivyo ameshauri DART kushirikiana na wataalamu wa Mipango Miji ili maeneo ya miundombinu yaingizwe kwenye mpango na zitakapopatikana fedha za kujenga miundombinu hiyo suala la fidia lisiwepo.
“Jukumu lenu ni kuhakikisha mipango hiyo jumuishi inakuwa ya muda mrefu ya miundombinu ya karakana, maegesho na vituo vya mabasi, hili likifanyika tutaokoa fedha nyingi za serikali kesho, mimi nikushukuru Mhe. Waziri kwa kuhakikisha halmashauri zinazopima maeneo kuweka kipaumbele kwenye miundombinu ya kijamii,”amesema.
Kuhusu Sheria inayosimamia DART, Mhe. Londo ametoa rai kuwepo na sheria inayolinda, kusimamia na kuendeleza Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ili kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na sio kanuni tu kama ilivyo sasa mradi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa mpaka sasa rasimu sheria ipo na inaendelea kupita kwenye michakato mbalimbali kabla haijawasilishes Bungeni kwa ajili ya mapitio. &&& View all comments
0 Comments