Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo akiwahutubia wananchi wa Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo
Wananchi na wana CCM kata ya Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Jioni ya Leo wamejitokeza Kwa wingi kwenye mkutano wa Hadhara wa katibu mkuu wa CCM Daniel Godfrey Chongolo .
Mkutano huo mkubwa umefanyika Katika viwanja vya soko la Ruaha Mbuyuni .
Akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo John Kiteve amesema Mapokezi hayo ni makubwa na wananchi wameonesha Imani Yao kubwa Kwa CCM na kuwa kujitokeza huko ni ishara tosha kuwa CCM .
Kiteve alisema kuwa furaha kubwa ya wananchi wa Ruaha Mbuyuni ni kuendelea kuona mradi wao wa Umwagiliaji unafanya kazi kutokana na changamoto kubwa ya mfereji kusombwa na Maji ya mvua .
Kiteve amepongeza ziara ya Chongolo ndani ya wilaya hiyo kwani imekuwa na manufaa makubwa Kwa wananchi wa Kilolo
SERIKALI ITAJENGA BARABARA YA MCHEPUKO MLIMA KITONGA -CHONGOLO
Kwa upande wake Katibu mkuu wa CCM) Daniel Chongolo amesema chama Chake kitahakikisha changamoto ya barabara ya Mchepuko kwenye Mlima Kitonga inafanyiwa kazi .
Chongolo alisema barabara hiyo ni muhimu na lazima iwe na barabara ya Mchepuko.
"Sisi tunajua umuhimu wa barabara ya Kitonga kuwa na Mchepuko kwani ni barabara muhimu sana Katika uchumi wa mkoa wa Iringa mikoa ya nyanda za juu kusini na Nchi za kusini mwa Tanzania hivyo changamoto hiyo anaichukua ili kufanyiwa kazi "
Pia katibu mkuu huyo ameuagiza uongozi wa Serikali mkoa wa Iringa kutatua kero ya vyumba vya madarasa Katika shule ya msingi Kidika kata ya Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo.
Alisema kuwa changamoto ya vyumba vya madarasa lipo ndani ya uwezo wa Serikali na litafanyiwa kazi Haraka iwezekanavyo .
Pamoja na changamoto ya vyumba vya madarasa pia ameagiza changamoto ya Maji safi na salama kwenye kitongoji hicho itafanyiwa kazi Kwa kuchimba kisima .
Pia Chongolo alisema changamoto ya gari la wagonjwa Katika eneo la kituo Cha Afya Ruaha Mbuyuni pamoja na chumba Cha kuhifadhia maiti kwenye kituo hicho Cha Afya zitafanyiwa kazi .
Hata hivyo alisema Magari yanayoletwa ni maalumu Kwa ajili ya wagonjwa na gari moja kati ya Magari matatu yatakayoletwa Kilolo ni kuajili ya ufuatiliaji na marufuku Magari hayo kutumika Kwa matumizi binafsi .
Akizungumzia Kuhusu changamoto ya skimu ya Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni ambayo imeharibiwa na mvua alisema ndani ya wiki moja wataalamu wa Umwagiliaji watafika ili kusaidia kuboresha skimu hiyo .
0 Comments