Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa, "Fatma Rembo" amewashauri wanachama wa CCM kuchapa kazi na kuendelea kukipigania chama hicho.
Fatma Rembo amesema hayo alipopewa nafasi ya kujitambulisha wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Kiongozi huyo wa UWT, amewaambia wanachama hao wasichoke kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
"Tupambane, kuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2025 na tuhakikishe viongozi wote wanatokana na CCM," amesema Rembo.
Amempongeza Katibu Mkuu, Daniel Chongolo kwa ziara yake Mkoani Iringa iliyolenga kuhamasisha uhai wa chama hicho na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Aidha, amempongeza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa kwa kuchapa kazi akikutana na makundi mbalimbali.
0 Comments