Wananchi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wameiomba serikali kuwapelekea chakula cha msaada ili kuokoa maisha yao kutokana na mnyama Tembo kuharibu mazao ya wakulima kwa asilimia kubwa.
Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Nachingwea, wananchi hao walisema kuwa Tembo wameharibu mazao mbalimbali katika mashamba yao hivyo kusababisha njaa kwa wananchi.
Walisema kuwa wanaimba serikali kuwapelekea chakula cha msaada kwa kuwa hawana chakula na hawana pesa za kununulia chakula kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Nachingwea wanategemea kilimo kuendesha maisha yao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa serikali inalitambua tatizo la Tembo kuharibu mazao ya wananchi hivyo wameanza mikakati maalumu ya kutafuta chakula cha msaada.
Moyo alisema kuwa walishalifikisha Jambo hilo la njaa serikali kuu hivyo wanasubili majibu kutoka serikalini ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi wa Nachingwea.
0 Comments