Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan ameshudia Utiaji saini mikataba ya kupeleka huduma ya Mawasiliano vijijini ambapo ameagiza Wakala wa Usambazaji Umeme vijijini (REA) kuhakikisha wanapeleka haraka umeme kwenye vitongoji ambapo Mradi wa Kusimikwa kwa Minara ya huduma za Mawasiliano umefika Mradi utakaogharimu jumla ya Fedha za kitanzania bilion 60.7 .
Akiongea leo jijini hapa Rais Samia Amesema Mradi huo unakwenda kutoa huduma bora za Mawasiliano katika Mikoa 26 Tanzania Bara.
Amesema ipo Changamoto ya upungufu wa umeme vijijini hali inayopelekea wananchi kushindwa kupata huduma hiyo ya Mawasiliano Hali inayopelekea kutokuwa na Maendeleo yao na. Taifa kwa ujumla.
Pia amezitaka halmashauri na Taasisi zote zinazohusika na Utiaji wa vibali kuhakikisha wanatoa vibali hivyo haraka ndani ya wiki moja na sio miezi kwa miezi.
" Najua kuna watu wazito Kutoa vibali hivyo kwa wale wenye makoti mazito sasa wavue makoti yao na waweze Kutoa vibali kwa sheria na taratibu zilizowekwa, "Amesema
Aidha Tarula na Mfuko wa Mawasiliano kwa UCSAF kukaa Pamoja ,kuongea na kuandaa barabara ni wapi mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wapi utapita.
MKURUGENZI WA USCAF
Akizungumza katika hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba amesema katika kuhakikisha wanafikisha huduma ya mawasiliano vijijini wanaenda kujenga minara 758 katika kata 713.
Amesema katika minara hiyo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) walishinda zabuni katika kata 104 na watajenga minara 104, Vodacom Tanzania amelishinda kata 190 watajenga minara 190, Airtel Tanzania walishinda kata 161 na watajenga minara 168 , Tigo walishinda zabuni katika kata 244 na watajenga minara 262 na Haloteli walishinda zabuni katika kata 34 na watajenga minara 34.
Aidha , amesema pia katika mkataba huo wanaenda kuongea nguvu katika minara 304 ambayo ilikuwa inatoa huduma ya 2G sasa itaanza kutoa huduma kwa 3G na maeneo mengine 4G.
“Lengo kubwa la kuanzisha UCSAF ni kupeleka mawasiliano maeneo ya vijijini na kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya mawasiliano bila vikwazo ambapo katika kuhakikisha hilo hadi sasa tumeshajenga minara nchi nzima .
Ameongeza kuwa :”USCAF Imepeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ambapo hadi sasa tumepeleka katika shule 4750.pia tunaendelea na mradi wa tiba mtandao lengo ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bila kwenda Hospitali.
Justina amefafanua kuwa lengo la mfuko ni kuhakikisha wanafikisha mawasiliano mipakani na katika mbuga za wanyama.
Naye Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye Amesema Jumla ya minara 758 inakwenda kuweka katika vijiji ambapo watanzania Milioni 8.5 wanakwenda kunufaika na Huduma hiyo ya mawasiliano.
MKUU WA MKOA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alisema minara hiyo ya mawasiliano itafanya Tanzania ifunguke Kimataifa.
Amesema mkoa wa Dodoma una maeneo mengi ambayo bado mawasiliano hayafiki hivyo kupitia minara 758 ambayo itajengwa na mkoa wa Dodoma itanufaika.
“Kupitia mradi wa mawasiliao kwa wote mkoa wa Dodoma unanufaika na minara 77 katika kata 56 na vijiji 202. Minara hiyo ilitumia zaidi ya sh.bilioni 11 kujegwa haya ni mafanikio makubwa na kufungua nchi kwa kiwango cha hali ya juu
"Sisi mkoa wa Dodoma tunakupongeza kwa kazi hii kuwa unayoifanya na sisi tulikuwa tunaandaa program ya kufuatilia minara hata tukiwa ofisini hivyo tunaamini kuimarika kwa huduma hii kutaifungua kila sekta..
CHONGOLO
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ameahidi kutoa kompyuta 50 kwa serikali lengo kuongeza chachu ya mafunzo kwa kutumia TEHAMA shuleni.
Chongolo amesema matumizi ya teknolojia yanaweza kuturahisihsia mambo na kuongeza chachu ya maendeleo.
“Kwa tukio hili muhimu la utiaji saini ujenzi wa minara ya mawasiliao kwa niaba ya CCM tunaipongeza serikali kwa kuchukua uamuzi wa msingi ambao unaenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2020/2025 kwa kiwango kikubwa.
Ameongeza kuwa :”Kwa niaba ya CCM tumeamua kuweka ndoano ilituvune kirahisi na kwa kuanzia CCM itatoa kompyuta 50 ili angalau kuweka chachu ya msukumo wa utekelezaji wa ilani katika teknolojia na mawasiliano katika shule zetu nchini.
0 Comments