NA MWANDISHI WETU, MTWARA
Zaidi ya vijana 82 programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) waliopo katika chuo cha kilimo mtwara MAT wametembelea katika taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo na kujionea aina mbalimbali a mbegu ikiwemo mbegu za zao la ufuta.
Akizungumza kituoni hapo Otilia Zakaria kutoka Mkoani Ruvuma alisema kuwa masomo hayo kwake yamekuwa na tija kubwa kwakuwa amekuwa akilima zao la ufuta kwa muda mrefu bila kujua mbegu bora wala kufuata kanuni bora za kilimo hicho.
“Nimeona aina za ufuta na kujifunza aina za mbegu na jinsi ya kufata utaratibu wa kupanda na kudhibti wadudu aina za mbegu nimeona tano lakini mbegu ya ziada na lindi 2000 kwa udongo wetu itafaa zaidi”
“Kwetu tunachangamoto ya ufuta kuharibiwa na wadudu tunaweza kudhitbi kabla haujawa mkubwa ambapo unachanganya na dawa na mbegu ninapomaliza mafunzo haya naenda kuwa mkulma bora na wakisasa zaidi”
Naye Mkurugenzi wa TARI Dk. Fortunus Kapinga alisema kuwa zipo tafiti za mazao mbalimbali zinafanyika katika taasisi hizo zikiwemo tafiti za zao la karanga na ufuta.
“sisi tunasimamia mazao ya korosho karanga na ufuta kitaifa ambapo vijana hawa watapata nafasi ya kujifunza na kuona aina mbalibali za mbegu za ufuta na karanga ili wanapojifunza kilimo bishara waweze kujua nini mahitaji ya soko mbegu gani bora zinaweza kuwafaa wakati gani zina sifa gani na wapi wanaweza kuzipata wapi”
kwa upande wake Mtafiti na Mratibu wa Programu za Ufuta kitaifa Joseph Mzunda alisema kuwa zao la ufuta kibiashara lina tija linakomaa kwa muda mfupi lakini pia zipo mbegu bora zenye sifa mbalimbali ikiwemo kuvumilia ukame.
“Tunajaribu kuona kama tunaweza kupata mbegu inayoweza kuzalisha mapema zaidi ili kunapokuwa na changamoto ya mvua isiweze kuwaathiri zaidi wakulima lakini kwasasa tunazo mbegu zinazofaa kulimwa katika maeneo mengi ya nchi” alisema Nzunda
Aidha Mtafiti wa zao la karanga kutoka Tari kituo cha Naliendele Said Ally alisema kuwa amewaelekeza vijaana hao kanuni bora za kulima zao karanga.
Ni vema wamefahamu kanuni bora za kilimo cha Karanga ndio maana tumewafundisha ili waweze kuzalisha kwa tija ili wakulima waweze kufanya kilimo chenyeh tija mpaka sasa zipo karanga za muda mfupi na muda mrefu ambazo zinahcukua siku 90-120” alisema Ally
0 Comments