NA THABIT MADAI, ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP
KATIKA Kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi, Jumla ya Miti 5000 inatarajiwa kupandwa katika Kijiji cha Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini (EBARR).
Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini unatekelezwa katika ya Simanjiro, Mpwapwa,Mvomero, kishapu na Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari huko Maruhubi Mjini Magharib Unguja, Mratibu wa Mradi wa EBARR wa Zanzibar, Alawi Haji Hija, alisema kuwa lengo la upandaji wa Miti hiyo ya Asili na Matunda ni lengo la kuhimili mabadilko ya tabianchi na kurejesha uoto asili na matumizi bora ya ardhi.
Pia alisema, kupitia mradi huo pia watajenga vitalu nyumba ambapo ni kilimo kimekuwa kikistahamili ukame.
Alisema,mradi huo kwa upande wa Zanzibar wanatekeleza kwa shehia tatu zilizoko katika kijiji cha Matemwe, ikiwemo shehia ya Matembe kijini, Matemwe mbuyu tende na shehia ya Matemwe Jugakuu.
Alisema, lengo la mradi huo ni kuimarisha uoto wa asili kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo alisema athari hizo zipo katika maeneo mbalimbali na kila eneo limekuwa na athari zake.
“Kwa upande wa matemwe ni maeneo ambayo yameathirika na kunatatizo kubwa la ukosefu wa mvua za kutosha na ukiangalia katika mazingira ya eneo lile kuna uharibifu mkubwa wa misitu” alisema.
Hivyo, alisema wataendeleo kurejesha hali hiyo sambamba na kuwapatia kipato wananchi kwa kuwawezesha kupata kipato chao bila ya hata kuharibu mazingira.
Hivyo, alisema mradi huo umekuwa unawasaidia wanajamii hata kupata kipato na kuwahimiza shughuli zao zisiwe moja kwa moja atika shughuli za kuharribu mazingira.
Alisema ili kudhibiti suala hilo, wamegenga majiko banifu ambapo yamekuwa yakitumia kuni chache kwa muda mrefu, jambo ambalo limekuwa likiwapa afueni miti iliyozunguka katika eneo hilo.
Aidha alisema pia kupitia mradi huo wamechimba visima sita vimechimbwa ili kuwezesha upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kilimo cha mbogamboga, wameviwezesha vikundi vya uvuvi kwa kuwanunulia boti sita za kisasa.
Nao, waandishi wa habari, wamesema watendelea kushirikiana na watendaji wa mradi huo ili kuona hali ya tabiachi inaendelea kuimarika sambamba na kuahidi kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Mradi wa EBARR unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika La Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP)ambapo utekelezaji huo ulianza mwaka 2018 na unategemewa kukamilika Februari 2024.
0 Comments