Na Titus Mwombe, Matukio Daima App KAGERA.
MKUU wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amewaonya wakuu wa taasisi za umma mkoani humo kuwa hayupo tayari kufanya kazi na viongozi, wazembe,wabadhilifu, wavivu na wanacholeweshaji miradi ya maendeleo mkoani humo.
Ameyasema hayo katika kikao maalumu wakati akiongea na wakuu wa taasisi za umma wa mkoa wa Kagera kilichofanyika leo katika ukumbi wa mkoa huo akiwa na lengo la kufahamu mipango waliyonayo wataalamu hao ili kuhakikisha mkoa huo unapiga hatua kimaendeleo.
"Tuko hapa Kagera kufanya kazi yawezakuwa wewe umezaliwa kagera au nje ya kagera tukishakutana hapa Kagera mambo mengine tunayaweka pembeni tunashughulika na jambo moja la kufanya kazi na kutimiza majukumu yetu kuhakikisha mkoa huu unatoka hapa hapa ulipo unasonga mbele kimaendeleo, mambo ambayo sitavulia kwa mtumishi yoyote ni uzembe,uongo,uvivu,ubadhirifu pamoja na ucheleweshwaji wa miradi kama kiongozi hawezi aombe uamisho mapema aondoke mapema" alisema Mwassa.
Aidha amesema kuwa wananchi wa mkoa wa kagera wanakiu ya kuona mkoa huo unapiga hatua kimaendeleo zaidi hivyo ni wajibu wao kama viongozi kuhakikisha wanasimamia miradi ya kimkakati kukidhi haja ya wananchi hao.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Kagera Toba Nguvila katika kikao hicho aliwataka wataalamu hao kuandaa mapema mipango na mikakati mahususi ya miradi ya kimaendeleo pamoja na maeneo mahususi ambapo miradi hiyo itajengwa baada ya bajeti za idara zao kupitishwa bungeni.
0 Comments