Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma.
SHIRIKA la Umeme Tanzania TANESCO kwa Mara ya kwanza imeandika historia kwa kusaini Mkataba wa kuzalisha Umeme kwa kutumia Umeme wa Jua wenye uwezo kuzalisha Megawati 150 za Umeme
Hayo yanesema leo jijini hapa na Mkurungezi Mtendaji wa shirika hilo Maharage Chande wakati wa Utiaji saini Mkataba wa kwanza wa Umeme wa Jua kishapu Mkoani Shinyanga.
Mkurungezi huyo Amesema Mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza zitazalishwa Megawati 50 na awamu ya pili utahusisha uzalishaji wa Megawati 100.
"Huu ni Mradi wa mkubwa kuwahi kutokea wa kuzalisha Umeme kwa kutumia jua hapa nchini na katika ukunda wa Afrika Mashariki," Amesema Chande
Na kuongeza " Mradi huu utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya hii ya kwanza zitazalishwa Megawati 50 na awamu ya pili utahusisha uzalishaji wa Megawati 100 na Mradi huo utatekelezwa na Kampuni ya SNOHYDRO CORPORATION kutoka China na Gharama za Mradi Hadi kukamilika kwake ikiwemo ulupaji fidia kwa wanaopisha eneo la Mradi Ni jumla ya kiasi Cha Shilingi za kitanzania Bilion 274.76.
Kwa Upande wake Waziri wa Nishati January Makamba amewapongeza wananchi wa Kishapu Mkoani Shinyanga huku akimshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwakuendekea kuifungua nchi na kuwezesha kupata Fedha hizo kutoka shirika la Maendeleo kutoka Ufaransa AFD.
Pia amewataka wananchi wa kishapu Mkoani Shinyanga kuhakisha wanatumza Mazingira ya Mradi huo ili ukalete tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla .
Waziri Makamba amesema katika mwaka wa Fedha ujao Serikali inakamilisha mkakati wa Umeme jadidifu ambapo mpaka Sasa wapo kwenye maandalizi mazuri
"Siku hizi Fedha nyingi za mikopo ya mitaji zinapatikana katika uwekezaji wa namna hii ya nishati hii hivyo Kama nchi hatuwezi kubaki nyuma hatuwezi kubaki nyuma katika Teknolojia mpya lazima tuwe na mkakati na sera zitakazotuwezesha kupata furasa nyingi za pesa zilizomo duniani,"amesema Waziri makamba.
Amesema kutokana na hatua hiyo Shirika la (TANESCO) linafanya tafiti na kuainisha ni maeneo gani panauwezo wa kupatika umeme wa Jua na upepo ili kuweza kuvuna Umeme wa kutosha na kuongeza afya kwenye grid ya Taifa.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amesema watatoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili mradi huo umalizike kwa wakati na kuwahudumia wananchi wa kishapu na watanzania kwa ujumla.
"Tunaimani kupitia Mradi huu wananchi wanakwenda kupata ajira na hata madhari ya mkoa wa Shinyanga utabadilika na kupitia Umeme huu shida ya kukatika kwa Umeme unakwenda kwisha,"
Na kuongeza" Mkoa wa Shinyanga ilikuwa na uhitaji mkubwa wa Umeme kwani Kuna migodi ya madini na dhahabu bila kusahau shule na hisptali zinazoendelea kujengwa," Amesema Mkuu wa mkoa huyo.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Judith Kapinga amesema Nishati ya Umeme ni Nishati nyeti hivyo umeme huo wa jua unakwenda kuongeza tija kwenye gredi ya Taifa na manufaa yake yataonekana baadae .
0 Comments