- Akemea ujanja ujanja asema mtumishi lazima awe wa kuongoza njia na kutoa Suluhu ya utatuzi wa migogoro*
RC Chalamila amesema hayo leo wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee kwa lengo la Kujitambulisha.
RC Chalamila amekemea ujanja ujanja katika utumishi wa Umma, Rushwa, Urasimu Katika utoaji wa huduma, vilevile amewataka kusimamia haki, usimamizi mzuri wa miradi, kuendeleza Utu, kutoa huduma bora kwa wateja, utatuzi wa migogoro na kuwa na Mawasiliano yanayofuata ngazi za uongozi kuanzia wa juu hadi wa chini.
Aidha RC Chalamila amesema kwenye utumishi ushirikiano na kuheshimiana ndio silaa kubwa ya mafanikio hivyo milango yake iko wazi kwa yeyote yule mwenye wazo au ushauri anakaribishwa.
0 Comments