Header Ads Widget

WANANCHI MSIUZE ARDHI OVYO- CHONGOLO

 

Katibu Mkuu wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameongoza harambee ya kumjengea nyumba Rose Nzelemera mwenyekiti wa CCM shina namba 4 Katika Kijiji la Ilambilole kata ya Kising'a Jimbo la Isimani  aliyekuwa akiishi nyumba ya Kupanga.

Hatua ya katibu mkuu Chongolo kuendesha harambee hiyo imekuja Mara baada ya taarifa ya shina hilo mbali ya mafanikio mbali mbali ya chama ila changamoto moja wapo ni mwenyekiti wao Kuishi Nyumba ya kupanga.


Kutokana na taarifa hiyo katibu wa itikadi na uenezi Taifa Sophia Mjema alianzisha harambee hiyo Kwa Viongozi wanawake waliokuwepo kwenye msafara wa katibu mkuu na kufanikiwa kupata Vifaa vya kuanzia ujenzi huo .

Miongoni mwa Viongozi waliochangia ni pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego,mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica Kessy ,Mhandisi Fatma Rembo ambae ni Mjumbe wa baraza la UWT Taifa ,Seck Kasuga,Zainab Mwamwindi mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa pamoja na yeye mwenyewe Mjema .


Hata hivyo Kwa uzito wa jambo hilo katibu mkuu wa CCM Chongolo kabla ya kuendelea na hotuba yake Kwa wana CCM na wananchi kwenye mkutano huo wa shina alilazimika kuendekeza pale alipoishia mwenezi Taifa .


"Huyo ni mwenyekiti Wetu wa CCM Shina hili namba 4 hapa Ilambilole na anafanya kazi kubwa Sana Kwa Sana ila haipendezi kuendelea Kuishi Nyumba ya kupanga Sasa nawainua Viongozi wachache hapo ili kumaliza Nyumba yake"alisema Chongolo .


Huku akimuinua mbunge wa Jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi Kwa kumtaka kumnunulia kiwanja mwenyekiti huyo na kuwaomba Wajumbe wa NEC Leonard Mahenda na Richard Kasesela wa NEC Taifa na Mnec wa mkoa wa Iringa Salim Abri Asas kuchangia Vifaa   na ufundi wa  Nyumba hiyo .


Huku Mjumbe wa kamati ya Siasa ya CCM  mkoa wa Iringa Dickson Mwipopo pia akiunga mkono zoezi hilo.



Wengine waliounga mkono ni pamoja na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini Costandino Kihwele  na wengine .


Chongolo mbali ya kuwashukuru wote waliojitokeza kuchangia ujenzi wa Nyumba hiyo alisema Nyumba hiyo anataka ikamilike haraka zaidi pindi atakapomaliza ziara yake mkoa wa Katavi atapita Kuizindua .


"Niagize ujenzi wa Nyumba hii uanze kesho maana pesa ya ufundi tayari MNEC Salim Abri Asas amekwisha toa na Vifaa vyote na kiwanja mheshimiwa Lukuvi amemnunulia " alisema 


Wakati huo huo Chongolo ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Iringa Vijijini kukamilisha andiko la kubadili eneo la malisho ya Mifugo lenye ukubwa wa heka 11,000 Katika kijiji hicho na  kuwa eneo la Kilimo Cha mpunga .



Katibu huyo mkuu alisema Mara baada ya Halmashauri kukamilisha zoezi hilo mkuu wa mkoa apewe andiko hilo tayari Kwa Utekelezaji wa Mabadiliko ya Ardhi hiyo toka malisho ya Mifugo kuwa ya Kilimo .



Mbunge wa Isimani Wiliam Lukuvi alisema changamoto kubwa ya wananchi wa Ilambilole ni ukame unaosababisha upungufu wa chakula hivyo iwapo eneo hilo litatumika Kwa Kilimo changamoto ya chakula inaweza kupungua kwani tayari Kuna mradi wa bwawa ambalo litatumika Katika Umwangiliaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI