Header Ads Widget

MWANAMKE AZIKWA KICHWA BAADA YA MWILI WAKE KULIWA NA MAMBA MTO LUKULEDI, LINDI

 



NA HADIJA OMARY_LINDI……….



MWANAMKE mmoja aliefahamika kwa jina la Somoe Saidi (65) mkazi wa Kijiji cha Nachui kata ya Nyengedi Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi amefariki dunia kwa kuliwa na mamba alipokwenda kuoga katika mto lukuledi

 

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na marehemu huyo inaeleza siku ya tukio mama huyo alikwenda mtoni kwa ajili ya kukoga na kuchota maji lakini baada ya muda kupita wanakijiji wengine walikwemda mtoni ndipo wakakuta ndoo ya maji  pamoja na nguo pembezoni mwa mto huo


“ Bila kutambua zile nguo na ile ndoo ni ya nani ila  walianza kutilia mashaka kuwa uwenda aliekuwepo eneo lile anaweza kuwa amechukuliwa na mamba kwani tofauti na vitu hivyo vilivyokutwa pia kulikuwa na damu damu  pamoja na mikwaluzo pembezoni mwa mto”

 

Kwa upande wake kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi ACP Alhaji Salim kabeleke amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema mai 24/2023 katika  mto lukuledi uliopo Kijiji cha Nachiu kata ya Nyengedi  halmashauri ya Mtama

 


Hata hivyo ACP Kabeleke  alisema kuwa mwili wa marehemu huyo ulipatikana siku ya tatu baadae baada ya kufanya msako kwa kushirikiana na askari wa maliasili huku mwili wake ukiwa umeliwa na mamba huyo na kusalia kichwa pekee

 

Aidha ACP Kabaleke amewataka wakazi wanaoishi na kufanya shughuli zao karibu na mto lukuledi kuwa makini na mamba huku akiwaomba kushirikiana na watu wa maliasili ili kutambua maeneo hatarishi ya makazi ya mamba hao

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI