Header Ads Widget

MWALIMU SEKONDARI YA KASANGA MUFINDI AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

 


Mwalimu wa shule ya Sekondari ya kasanga Wilaya ya Mufindi, Saidi Riziki Kikoti ( 34) amehukumiwa kifungo cha Miaka 30 Jela huku akitakiwa kulipa fidia ya sh 5 Milioni baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kumbaka Mwanafunzi wa shule hiyo mwenye umri wa Miaka (15) na kumsababishia kupata ujauzito.

Kesi hiyo ya jinai namba 31 ya mwaka 2023 ambayo hukumu yake imetolewa jana jumatatu Mei 15,2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Akizungumza na Mwananchi leo jumanne Mei 16,2023 na Hakimu Mfawidhi Mwandalizi wa Mahakama hiyo ,Benedict Nkomola ambapo amesema kuwa Mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo January 14,2023 mwaka huu huko katika kata ya kasanga Wilayani hapa.

 Aidha Hakimu huyo amesema kuwa mshtakiwa ameshikiwa kwa kosa la ubakaji ambalo ni kinyume na kufungu cha sheria 130 (1)(2)(e) na kufungu 131 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Hakimu huyo amesema kuwa upande wa mashta ulieleza mahakamani hapo kwa siku ya tukio mshtakiwa alimuomba Mwanafunzi huyo kuwa akimaliza shughuli zake basi aende nyumbani kwake.

Hakimu huyo amesema kwa mujibu wa muhanga huyo alieleza mahakama kuwa baada ya kuambiwa hivyo alienda hadi nyumbani kwa Mwalimu huyo na alipofikia alimuomba akingie ndani chumbani kwake kisha kuomba waweze kufanya mapenzi.

"Baada ya kufanyiwa kitendo hicho hali ambayo ilipelekea kutoona siku zake kama ilivyokawaida alimfuata mshtakiwa na kumeleza hali ambayo anajisikia lakini alimjibu kwamba hali hiyo inatokana na mabadiliko ya kimwili."Amesema muhanga huyo.

Baada ya kuambiwa hivyo huku tumbo likiendelea kukuwa hadi pale baadhi ya walimu wa shule hiyo walipotia shaka kwamba Binti huyo atakuwa ni mjamzito ndipo wanachukuwa uamuzi wa kwenda kumpima katika kituo cha afya kasanga ambapo majibu ya vipimo alibainika anaujauzito.

Kwa upande wake mshtakiwa Kikoti alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kuhusika na ujauzito huo.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakari wa Serikali Yahaya Misango alitoa mapendekezo mahakamani hapo kutoa adhabu kali ya viboko na kifungo cha Miaka 30 Jela kwa mshtakiwa kutokana na vitendo hivyo kukithi katika Wilaya ya Mufindi.

"Niombe Mahakama mshtakiwa apewa adhabu kali ikiwemo ya viboko pamoja na kifungo cha Miaka 30 Jela ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo kutoka vitendo hivyo." Amesema Misango

Hata hivyo Hakimu huyo amesema kuwa kwa kuzingatia hati ya mashtaka iliyoletwa hivyo mahakamani ametoa adhabu ya kifungo cha Miaka 30 Jela lakini pia ametoa amri kuwa Mwanafunzi huyo aweze kulipwa fidia ya sh 5 Milioni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS