Header Ads Widget

MAWAKALA WA MAKAMPUNI MAKUBWA 370 YA WATALII KUKUTANISHWA JIJINI ARUSHA KATIKA MAONESHO YA KARIBU KILIFAIR



Teddy Kilanga


Arusha


Makampuni zaidi ya 370 ya watalii yenye wanunuzi wa bidhaa za utalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kufika Arusha nchini Tanzania katika maonesho ya utalii kupitia Karibu Kilifair inayotarajiwa kuanza Juni 2,2023 kwa lengo la kujionea vivutio vilivyopo na kwenda kuvitangaza katika Mataifa yao.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair ,Dominick Shoo alisema ujio wa makampuni hayo ni moja ya kuwa mabalozi wa kutangaza vivutio vilivyopo nchini ambapo kupitia maonesho ya Karibu Kilifair itawasaidia wananchi kupata fursa mbalimbali za biashara ya utalii.



"Katika miaka yote tuliyofanya haya maonesho ya Karibu Kilifair tumefanikiwa kuleta watalii wa nje zaidi ya 500 kwa kila mwaka na hii ni sehemu kubwa ya kuongeza mabalozi wa kuvitangaza vivutio vyetu vilivyopo Tanzania,"alisema Shoo.


Makamo Mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji Wawatalii nchini (TATO) Henry Kimambo alisema amonesho hayo ni chachu ya kukutanisha wadau wa sekta ya utalii wa nchi mbalimbali duniani ambapo utasaidia kufikia lengo la kufikia Watalii milioni tano kufikia mwaka 2025.


"Hii ni platform ambayo sisi wadau wa sekta ya utalii ndio mahali tinaweza kufanya marketing,promotion  pamoja nakuongeza ufahamu wa kutosha katika masoko ya utalii,"alisema Kimambo.


Afisa masoko Mkuu wa Tasisi ya fedha ya CRDB ,Boma Raballa alisema biashara ya utalii imechangia mapato la Taifa kiasi cha sh. 2.4 bilioni fedha za marekani ambapo ni mchango wa uwezeshwaji wa wafanyabiashara wa utalii uliofanywa na benki hiyo.


"Benki ya CRDB imekuwa na mchango mkubwa kwa wafanyabiashara wa utalii ambapo ilianisha kadi maalumu ya kusaidia watalii kufanya malipo yao bila vikwazo vyoyote,"alisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS